MASHINDANO YA REDE YAZINDULIWA KATA YA PUGU
Na Mwandishi wetu Dar
Mashindano ya Rede na mpira miguu yamezinduliwa Kata ya Pugu Station kwa kushirikisha timu 17 za kata ya Pugu Station ikiwemo Pugu mpakani, kirumba, kibiriko na Msimbazi.
Akizungumza katika uzinduzi wa Rede Cup Afisa Mtendaji wa kata ya Pugu Station Iginas Maembe alisema jumla ya timu 14 zimeshiriki Mashindano hayo yaliozinduliwa rasmi leo Juni 22/2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Afisa Mtendaji wa kata ya Pugu Station Iginas Maembe alisema dhumuni la Mashindano hayo kukuza vipaji na kujenga afya na Mahusiano kwani michezo ni afya .
"Mashindano haya yanachezwa viwanja vya Mnadani na Bangulo ujumbe wa Mashindano haya mwaka huu"Tulithi mazuri tujenge kesho" dhumuni lingine kuwakumbusha wananchi nchi yetu inaelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka huu mwezi Octoba hivyo wananchi wajipange kuchagua viongozi sahihi watakaoleta maendeleo " alisema Iginas
Mtendaji Iginas Maembe alisema katika mashindano hayo ya Rede mshindi wa kwanza mbuzi wawili,mshindi wa pili mbuzi mmoja na tatu jezi.
Mtendaji Maembe aliwataka wakazi wa Pugu Station kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya michezo nchini iweze kusonga mbele kwani michezo ni afya pia ni ajira.
Aidha alisema dhumuni lingine la michezo hiyo kuweza kuibua vipaji mbalimbali watakaoweza kuchukuliwa katika timu za Wilaya,mkoa na Timu ya Taifa.
Comments
Post a Comment