MWENYEKITI UVCCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA ATIA NIA KUGOMBEA KAHAMA



Aliyekua Mwenyekiti wa Uvccm Vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Dodoma Salum Ismail amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Octoba kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini amesema kuwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan ameweka mazingira rafiki kwa vijana kuweza kugombea .

Amesema kuwa, aametia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kahama mjini mkoani Shinyanga.

Amesema kuwa lengo la nia ya kugombea ni Kwa ajili ya kuwaketea maendeleo Wananchi wa Kibaha mjini kwani kupitia fursa nyingi zilizopo jimboni huko ikiwemo migodi ya Madini.

Katika hatua nyingine Salum amekemea wanasiasa na wanaharakati wanaochochea uvunjifu wa Amani Nchini hivyo amesema kuwa watahakikisha wanapambana nao.

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Rais Samia kutokana na mazuri aliyoyafanya.

Aidha, amesema Rais  Samia amepita katika mapito mengi lakini amehakikisha hali ya usalama wa Nchi inakuwa vizuri.

"Sisi kama makanda na vijana wasomi na watanzania atupo tayari kuona RAIS anabezwa kwa vyovyote vile,  hatupo tayari kuona mtu mwenye viashiria vya uvunjivu wa amani katika nchi ya Tanzania".

Miradi yote ya kimkakati imetekelezwa na imekamilika, tatizo la umeme, miundombinu ya barabara imetanuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI