MERY MTEGA AJITOSA UDIWANI VITI MAALUM ILALA


Na Heri Shaaban (CCM ILALA)

KADA wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Mery Mtega, amechukua fomu ya kugombea Udiwani wa viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala mkoa Dar es Salaam. 

Mery Mtega, alichukua fomu hizo za kugombea Udiwani wa viti Maalum Juni 30 na kurejesha Julai Mosi Ofisi za Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala .

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mery Mtega ,alisema yeye ni kada wa chama cha Mapinduzi chimbuko la Umoja wa Vijana wilaya ya Ilala ambapo kabla kuomba nafasi ya udiwani alikuwa na nyazifa  mbali mbali za uongozi ikiwemo UVCCM. 

Mery Mtega, alisema amejipima ameona anaweza katika kuwatumikia wananchi kupitia umoja wanawake UWT  chama chake kikimteua kikampa ridhaa baadae aweze kuleta maendeleo na kuwainua kiuchumi wanawake wezake.

"Wanawake ni jeshi kubwa dhamira yangu kubwa kuwa kiongozi nimejipima nimeona naweza kuwatumikia nikipata ridhaa  nitaleta maendeleo makubwa nimsaidie Rais wangu Dkt samia suluhu Hassan wanawake sasa hivi Jeshi kubwa" alisema Mery. 

Mery Mtega alitaja nafasi alizotumikia ndani ya chama cha Mapinduzi UVCCM,Mjumbe mkutano mkuu mkoa,Mjumbe wa Baraza Wilaya  ,Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na mjumbe wa Kamati ya ujenzi.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI