NAHODHA MUSSA ATEMBELEA BANDA LA TASAC ATOA WITO HUU

 




Na Mwandishi wetu 

Mwenyekiti wa bodi ya wakurungezi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ) Naodha Mussa Mandia ametembelea banda la TASAC lililopo katika maonyesho ya biashara ya 49 ya kimataifa yanayoendelea Sabasaba.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo Nahodha Mussa amesema kuwa shirika hilo limeshiriki katika maonyesho hayo kwa lengo la kutoa elimu.

"Akizungumzia kuhusu maonesho ya Sabasaba amesema TASAC inashiriki katika maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi inavyohakikishia usalama na ulinzi wa bandari zote nchini"

Amesema kuwa, shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema litaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya  usalama wa usafiri majini jinsi  unavyochagia katika uchumi wa nchi katika kukuza pato la taifa.

Hata hivyo, Kapteni Mandia  amesema hali ya usalama wa bahari ni shwari na TASAC imekuwa ikishirikiana na vyombo usalama katika maeneo hayo kupitia vyombo vya ulinzi na usalama.

Ameongeza kuwa, TASAC  ina jukumu la kudhibiti na kusimamia usalama, ulinzi wa usafirishaji majini ambao ni kiungo muhimu katika kukuza uchumi.

"TASAC inayo majukumu mawili moja la Udhibiti na lingine kuhamasisha watu kushiriki katika ulinzi na usalama na usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji"amesema Nahodha Mussa.

Hata hivyo, amesema mengine ya TASAC ni pamoja na kuhakikisha meli zote zinazotia nanga kwa ajili ya kuleta bidhaa mbalimbali nchini zinakuwa salama pamoja na kulinda mazingira ya bahari.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI