SHABANI MUSSA AREJESHA FOMU
Julai 1,2025, Shabani Mussa (Mwancelele), ambaye ni Diwani aliyemaliza muda wake wa kulitumikia kwa bidii na uaminifu wananchi wa Kata ya Pugu Stesheni, amerudisha rasmi fomu ya kugombea tena nafasi ya udiwani kwa kata hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua hiyo inaashiria nia thabiti ya Mwancelele kuendeleza miradi ya maendeleo, kusimamia maslahi ya wananchi, na kuimarisha mshikamano wa kijamii uliokuwepo katika kipindi chake cha awali.
Comments
Post a Comment