RAGI AWASHAURI WAJUMBE WA CCM KUELEKEA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA.

 


Na Mwandishi wetu, Dar 

Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga Ragi Samwel amewakumbusha Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi  kuhakikisha wanachagua viongozi waadilifu,Waaminifu na wenye nia thabiti ya kuwaletea maendeleo Wananchi.

Ragi ameyasema hayo leo Agost 3,2025 jimboni Ukonga ikiwa ni siku ya kuhitimisha kampeni za watia nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo amebainisha kuwa ni vyema wajumbe wa Chama hicho kujenga umakini wa kuchagua mwakilishi atakaye wajibika moja kwa moja kwa Wananchi badala ya maslahi binafsi.

Aidha amesema kuwa katika kinyang'anyiro hicho wajumbe wanapaswa kutazama zaidi maaslahi ya wananchi wa Ukonga katika kutatua changamoto zinazolikabili Jimbo hilo ikiwemo miundombinu ya Barabara,Afya na Elimu

"Nawaomba wajumbe wote wenye dhamana ya kupiga kura kuchagua viongozi sahihi na wenye mapenzi ya dhati na Jimbo letu,ili kuleta tija ya maendeleo" amesema Ragi. 

Uchaguzi wa kuwapata wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ngazi za Ubunge na Udiwani  kupitia kura za maoni unatarajiwa kufanyika hapo kesho nchi nzima.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI