ROTARY CLUB OYSTERBAY YAWEKA KAMBI YA MATIBABU BURE UKONGA

 


Na Mwandishi wetu 

Rotary Club  Oysterbay Dar es salaam kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya leo wameweka kambi ya  matibabu bure ikiwemo upimaji wa Saratani ya uzazi, tezi dume, macho, malaria, masikio, VVU pamoja na kutoa ushauri nasaha.

Kambi hiyo imewekwa katika  Shule ya Msingi Mzambarauni iliyoko Ukonga Gongolamboto Jijini Dar es salaam huku matarajio ya kuona wagongwa ikiwa ni 3500  kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wazee, wanafunzi na watoto.


Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 9,2025 Jijini Dar es salaam Muandaji wa Kambi ya Matibabu hiyo, Hilu Bura amesema wamejikita zaidi kutoa huduma kwa Jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo Afya, elimu pamoja na maji.

Ameongeza kuwa, zoezi hilo limepokelewa vizuri kwani walijiwekea lengo la kuhudumia watu  Elfu tatu miatano lakini mpaka sasa wanakaribia na kufika lengo hadi kuzidi 

"Tumekuja na madaktari bingwa wanawake na wanaume ambao wanatoa huduma za matibabu ya meno, ngozi, masikio, macho hivyo tumechagua kusaidia jamii kwa upande wa Afya kwa kuwa tunatambua siyo wote wanaoweza kumudu gaharama za Matibabu"amesema Hilu

 


Kwa Upande wake, Makamu wa Rais wa  Rotary Club Tanzania, Paul Muhato amebainisha kuwa wamekuwa wakitoa huduma hiyo ni mwaka wa nane kuisaidia jamii kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali ikiwemo Pepsi, CCBRT na SGA 

"Tumefanya hii huduma tangu 2018 masala ya Afya ni moja ya kipaumbele chetu ila pia tunasaidia masuala ya Elimu na tunatoa huduma hii mara mbili kwa mwaka tuna watu zaidi ya Milioni tatu ambao wamekuwa wakijitole kuisaidia jamii" amesema Muhato.


Wakizungumza na Habari Plus kwa nyakati tofauti wanufaika wa kambi hiyo wamesema wanashukuru Rotary kwa kuwaletea huduma hiyo karibu kwani wamewasaidia wananchi wengi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI