WANANCHI WAKARIBISHWA BANDA LA WIZARA YA NISHATI NANENANE DODIMA
Kufahamu fursa na miradi inayoendelea kutekelezwa
Wizara ya Nishati imeendelea kukaribisha wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Fredrick Marwa, Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati amesema katika maonesho hayo Wizara inaeleza kuhusu kazi mbalimbal zinaoendelea kufanyika ikiwemo za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bonde la Eyasi Wembere
Marwa amesema wananchi watakapofika katika Banda la Wizara ya Nishati pia watajionea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Wizara pamoja na Taasisi zake ikiwemo TANESCO, EWURA, REA na TPDC.
Comments
Post a Comment