Posts

Showing posts from May, 2026

LONDO - VIPIMO SAHIHI NI MSINGI WA UCHUMI WA VIWANDA NA TEKNOLOJIA

Image
  Na Habar Plus Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha mifumo ya vipimo nchini ili kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa, kukuza viwanda na kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea sayansi na teknolojia. Mhe. Londo ametoa kauli hiyo leo Mei 20,2026 jijini Dodoma wakati akifunga rasmi maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambapo amesisitiza kuwa maendeleo ya viwanda, biashara na huduma bora hayawezi kufikiwa bila uwepo wa vipimo sahihi na vinavyoaminika. Amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kisera na kisheria ili kuwezesha biashara, kuvutia uwekezaji na kuongeza ufanisi wa sekta binafsi kwa kuzingatia matumizi ya vipimo vinavyokubalika kitaifa na kimataifa. “Hakuna biashara yenye uaminifu bila vipimo sahihi, hakuna viwanda vinavyoweza kushindana kimataifa bila mifumo sahihi ya vipimo, na hakuna sera bora bila taarifa sahihi zinazotokana na sayansi ya vipimo,” amesema M...