MATHAMANI - SIJAKATAA UTEUZI



Na mwandishi wetu,HPMedia, Kigoma

Aliyekua Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Dinah Elias Mathamani amesema hajakataa uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani kigoma aliyoteuliwa na Rais wa Jamhuribya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan uliofanyika January 25, 2023.


Kauli hiyo ameitoa  January  31 mbele ya waandiahibwa habari mara baada ya kula kiapo cha uongozi kwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya mbele ya mkuu wa Mkoa wa kigoma Thobias Andengenye katika ukumbi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma.


Amesema kuwa, amesikitishwa na taarifa zilizokua zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii ya kuwa amekataa nafasi ya uteuzi aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kudai kuwa hazina ukweli wowote bali amefurahishwa sana na uteuzi huo na kuwa yupo tayari kuitumikia katika kiapo cha maadili ya uongozi.


"Baada ya majina kutangazwa na kuona jina langu ni mmoja wa wateule nilifurahi na nikaanza kufanya mawasiliano na viongozi wa Wilaya yangu na kujiandaa na safari ya kuja kwenye kituo changu cha kazi, niliona ni nafasi ya pekee kwangu na ninamshukuru sana Rais Samia kwa nafasi hii aliyonipa ya kuwatumikia wananchi"amesema DC Dinah.


Ameongeza kuwa, imani aliyopewa na Rais Samia ya kumteua kuwatumia wananchi atahakikisha anaitendea haki kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuleta maendeleo katika Wilaya hiyo na kusimamia ilani ya chama cha Mapinduzi ili itakapofika mwaka 2025 wapate cha kuwaeleza wananchi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma kuendelea kusimamia suala la ulinzi na usalama kwenye Wilaya zao kwani wahamiaji haramu wamekuwa wakiingia kupitia njia ambazo siyo za halali hivyo amewataka waweke uthibiti wa njia hizo ambazo si halali kwa wahamiaji kuingia.



"Rais amewaamini akijua uwezo wenu,mtumie vizuri mamlaka mliyonayo huku mkitambua majukumu yenu yanagusa maisha ya wananchi,wahamasisheni wananchi wajiunge na bima ya afya inayokuja bima ya afya kwa wote na bima zingine ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao"amesema Andengenye.


Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI