DC MPOGOLO AWATAKA WATENDAJI WASIWE KIKWAZO KWA SERIKALI


Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka watendaji wa wilaya ya Ilala kuwa karibu na Viongozi wa chama na Serikali huku akiwasisistiza wasiwe sehemu ya vikwazo katika kuleta maendeleo .

Wito huo ameutoa alipokua katika ziara ya kujitambulisha kwa watendaji na viongozi wa chama Tarafa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo amesema dhumuni la ziara hiyo kujitambulisha ,kujenga Mahusiano pamoja na kutatua kero mbalimbali zilizopo Wilayani humo .

"Naomba Watendaji wa Tarafa ya Ilala mshirikiane na chama na Serikali katika kujenga mahusiano pamoja na wananchi msiwe sehemu ya vikwazo ndani ya Wilaya Ilala  " alisema Mpogolo .

Aidha, amewataka Watendaji kushikamana na Serikali kutumikia wananchi katika utekekezaji wa Ilani katika kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kusimamia miradi ya Maendeleo ikiwemo ya sekta ya afya na sekta ya Elimu .

Hata hivyo, amewataka watendaji hao endapo kutatokea mtu amekosea basi wakosoane kwa staha na kwa kupitia vikao vilivyowekwa badala ya kusemana katika vijiwe na mikutano ya Wananchi .



Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji, alimpongeza Mpogolo kwa mada nzuri Semina elekezi amewapatia Watendaji na Viongozi wa chama Ili kila mtu aweze jua Majukumu yake .


Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ilala Habibu Nasser alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala watashirikiana naye katika utekekezaji wa Majukumu yake ya Chama na Serikali .

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI