SELEMANI KIDUNDA AACHA SINTOFAHAMU KUTOFIKA KUPIMA UZITO PAMBANO LA KESHO


Na Magrethy Katengu,HPMedia, Dar 

Bondia Selemani Kidunda ameacha sitofahamu kwa Mpinzani wake Raia wa (DRC)Patric Mukala baada ya kutojitokeza kupima uzito ikiwa ni maandalizi ya  siku moja ya Pambano la ngumi za kulipwa linalotarajiwa kufanyika Februari 24 2023 kuanzia saa mbili usiku.

Akizungumza mara baada ya kupima uzito Mabondia wengine Mkurugenzi wa Kampuni Kemmon Agency ambaye pia ni  Promota wa Pambano hilo Sada Salim amesema  amesikitishwa sana na kitendo alichofanya Selemani Kidunda kwani walishasainiana Mkataba hivyo Pambano lipo palepale na asipotokea atatakiwa kulipa fedha alizopewa na fidia kutokana na kukiuka Mkataba wa makubaliano yao.

Sitofahamu hii imekuja baada mzani wa Kidunda kupanda jukwaani na kupima uzito lakini baada ya mshereheshaji wa zoezi hilo kupitia siyo yeye wala wapambe wake hali iliyomlazimu kwa muda Mpinzani kupima uzito mwenyewe na kutofanya (Face off) mpaka anaondoka uwanjani Kidunda hakutokea

"Selemani Kidunda acha Woga njoo uwanjani uonyeshe Umwamba wako ulingoni usiogope kupigwa hata Thaison alivuma sana kushinda kila Pambano lakini aliwahi kupigwa acha janja janja tunataka tuone vitasa "amesema Promota Sada 

 Katibu wa kaminsheni wa ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC)Yahya Poli amesema  mpaka leo hawana taarifa yeyote ya Selemani Kidunda kufika hivyo kulingana na sheria ya ngumi za kulipwa hivyo ajitokeze kupima uzito mbele ya Mpinzani wake na aingie kwenye Pambano hilo hapo kesho.

"Itakapofika saa nane na nusu Mchana kama Selemani Kidunda hajatokea kupima uzito au kutoa taarifa zenye mashiko Pambano lake litafutwa ambalo kimsingi ndiyo kuu hivyo atachukuliwa sheria kali ikiwemo kulipa gharama au fidia "amesemaYahya.

Aidha wito umetolewa Kwa wanaopenda burudani hiyo kununua tiketi za kuingia katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kutazama mubashara Mpambano huo kupitia Azam Media ni kuwani Mkanda wa ABU Uzito wa Super Middle

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...