SIMBA YASEPA NA MILL 35 ZA RAIS DKT SAMIA
Na Mwandishi wetu HPMedia
Klabu ya Simba nchini Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuichapa mabO 7 timu ya Hoyora Fc ya nchini Guinea.
Simba imepata ushindi huo katika mchezo wake wa hatua ya makundi uliochezwa katika uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam leo Machi 18 ambapo wanaweka historia ya kuingia kwenye nafasi hiyo kwa mara ya nne.REPORT TH
Simba imefanikiwa kutinga hatua hiyo ikiwa nafasi ya pili na kujizolea pointi tisa huku Raja Casablanca ya Morocco ikiwa katika nafasi ya kwanza kwa pointi 13.
Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Clatous Chama (3) dakika ya 10, 36 kwa penalti na dakika ya 70, Jean Baleke akishinda magoli mawili Dakika ya 32 na 65, huku Sadio Kanoute akishinda magoli mawili dakika ya 54 na 87.
Ushindi huo wa Wekundu wa Msimbazi wanafanikiwa kujizolea milioni 35 zilizoahidiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akinunua kila bao linalofungwa kwenye michuano hiyo ya kimataifa kwa milioni 5.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wake wa kwanza uliochezwa ugenini dhidi ya Hoyora Simba walikubali kichapo cha bao 1-0.
Comments
Post a Comment