ACT YATOA HOJA 7 KWA SERIKALI

Na Magrethy Katengu,HPMedia,Dar 

Chama cha ACT Wazalendo kimetoa hoja 7 mara baada ya hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mapitio ya kazi na mwelekeo wa serikali na makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 hoja ikiwemo hali ngumu ya maisha,suala la ukosefu wa ajira,kukosekana kwa utaratibu wa kukabiliana na maafa ,kuchelewa kwa Miradi ya kimkakati.

Hoja hizo saba zimetolewa  leo Jijini Dar es saalam Waziri Mkuu kivuli chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu wakati akichambua Hotuba ya Ofisi  ya Waziri Mkuu kuhusu mapitio ya kazi na mwelekeo wa serikali makadirio ya matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 iliyowasilishwa Aprili 05 2023 Bungeni na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ambapo amesema Serikali iliyo chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inahitaji Mabadiliko makubwa ya kiuchumi hivyo wametoa hoja zao zifanyiwe kazi.

Dorothy akifafanua hoja ya hali ngumu ya maisha amesema kutokana na Mabadiliko ya hali ya hewa serikali iangalie na namna ya kununua chakula cha kutosha angalau miezi 3 kutokana chakula kitakachovunwa mwaka huu ili kujiandaa na upungufu wa chakula kutokana na ukweli kuwa maeneo mengi nchini uzalishaji unaweza ukawa siyo mzuri hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema

"Hatua hii ya kunusuru nchi na janga la ukosefu wa chakula na kusababisha njaa serikali kujenga uwezo wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Kwa kutenga bajeti ya kutosha ya kununua chakula (Tan million 1.5 za mahindi ,Tani laki 5za mpunga ,maharagwe Tani milioni 1) na kuwezesha Bodi ya mazao mchanganyiko kununua na kusambaza katika maeneo yatakayokuwa na uhaba wa chakula"amesema Semu

Hata hivyo ameishauri serikali iweke mazingira bora Kwa wakulima wadogo Ili kuongeza uzalishaji zaidi Kwa kuendelea kutoa ruzuku katika mbolea na kusimamia usambazaji wake kuhakikisha usalama wa ardhi kwa wakulima na kushughulikia migogoro ya ardhi.

Sanjari na hayo akifanua hoja nyingine ya ukosefu wa ajira na maslahi ya Wafanyakazi amesema athari ni janga kubwa sana katika Jamii yetu husababisha ikiwemo kuongezeka wimbi la umasikini na utegemezi, kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili na uhalifu ikiwemo vitendo vya wizi,ukahaba,unyang'anyi,uporaji,kuongezeka kupendeleana na rushwa katika utolewaji wa ishughulikiwe mara Moja

Aidha, amesema katika sekta mbalimbali kumekuwa na uhitaji wa wataalamu hivyo na Vijana waliohitimu wapo wengi mtaana hawajui pa kwenda serikali iangalile suala hilo kwa jicho angavu 

"Tumedhuhudia mahitaji makubwa ya wafanyakazi na watumishi tena kwenye sekta nyeti kama vile Elimu,afya na kilimo lakini serikali hajaweka Mkazi kabisa kwenye kuhakikisha sekta hizo zinapata wataalamu na watumishi licha ya kuwepo wataalamu waliosomeshwa Kwa gharama kubwa na kuwaacha mtaani hivyo tunashauri serikali kupatia ufumbuzi jambo hilo "amesema Dorothy 

Aidha Serikali imeshauriwa kujenga uwezo wa kibajeti kununua vifaa vya kisasa vya uokoaji kujenga uwezo Idara ya maafa na taasisi zilizo chini yake kununua vifaa vya kuongeza ufanisi wa usimamizi wa kutumia Teknolojia ya Kufuatilia maafa sehemu mbalimbali za nchi

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI