UWT KUNDUCHI YATOA ELIMU YA UKALITI NA MAADILI MEMA KWA WANAFUNZI 5000




Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar 

Umoja wa Wanawake Kata Kunduchi (UWT) imewajengea uwezo wanafunzi zaidi ya 5000kutoka Shule ya Sekondari Kondo, Shule za Msingi Pius Msekwa na Shule ya Msingi Kunduchi lengo ikiwa ni kuwataka watambue cha kufanya hasa wanapotendewa ukatili wa kijinsia ama wanapokutana nao.

Akizungumza na wanafunzi katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kunduchi Twilumba Jane Balama amesema watahakikisha wanawafikia wanafunzi wote katika shule zilizopo kwenye Kata ya Kunduchi ili kuisaidia Serikali kupambana na ukatili na hasa kutengeneza kizazi kilicho bora zaidi kwa maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.

Amesema kuwa, lengo kufanya ziara hiyo ni kutokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia  kuongezeka siku hadi, hivyo wameona ni jambo jema kuanzia mashuleni ambako ndio kuna wahanga wakubwa.

"Tumeona tuanzie mashuleni kwani watoto wengi ndio waathirika wa vitendo vya ukatili  kwa hiyo tumewafikia watoto wasiopungua 5000 na kuzungumza nao kuhusu maadili mema na namna ya kutambua ukatili wa kijinsia na nini cha kufanya endapo watakutana na ukatili"amesema Twilumba. 

Hata hivyo, amewashukuru wadau wote kwa kuweza kufika kuungana nao katika kutoa elimu hiyo ya malezi na maadili bora kwa watoto waliopo mashuleni ambapo itaweza kuwafikia watoto wengi zaidi.

Aidha, katika ziara hiyo waliambatana na Katibu UWT Wilaya ya Kinondoni Aziat Juma, Mjumbe Halmashauri Kuu CCm Mkoa wa Dar es Salaam Francis Nanai, Diwani wa Kata ya Kunduchi  Michael Urio, Dawati la Jinsia Mkoa wa Kawe, mwakilishi kutoka SMAUJATA Irene Mashine, Afisa Ustawi wa jamii na Afisa Maendeleo Kata ya Kunduchi ambao wote walikuwa wazungumzaji katika ziara hiyo.

Mbali na kuwajengea uwezo, UWT Kunduchi waliwapa Motisha watoto hao kwa kuwapa zawadi (counter books, mathematical sets, kalamu na penseli) wanafunzi walioibuka Tano bora katika Kila darasa.

Aidha Michael Urio ambae ni Diwani wa Kata hiyo,ametoa wito kwa wakuu wa shule kuandaa mkutano na wazazi ambapo Uwt Kunduchi pamoja na wadau wote waliofika kuwajengea uwezo watoto hao waweze kuzungumza na wazazi kuhusu malezi bora kwa watoto wetu.



Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI