DCEA YABAINI MBINU MPYA USAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA, WANAWAKE MATATANI

 

Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar 

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) imewataka wanawake nchini Tanzania kuwa makini wanapoingia katika mahusiano ya kimapenzi na raia wa kigeni ili kujiepusha kuingia kwenye matatizo ya usafirishaji wa madawa ya kulevya.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mamlaka hiyo kumebaini mbinu mpya zinazotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambao huwatumia wanawake katika usambazaji wa dawa hizo bila wao kujua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar er Salaam kamishna jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo amesema mbinu hiyo mpya wameigundua baada ya DCEA kufanya operesheni katika kipindi Cha miezi miwili na wiki tatu ambapo ilibaini wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakiwatumia wanawake kwa ajili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Amesema kuwa, hadi sasa jumla ya wanawake zaidi ya 20 wamekamatwa na tayari  wapo gerezani kutokana na kukutwa wakiwa wamedhihifadhi dawa hizo ambapo tayari wamefikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea.

Aidha amesema kuwa kutokana na kuibuka kwa mbinu hiyo mpya wanawake wanapaswa kuwa makini kwani hali hiyo inaweza kuwasababisha kuingia katika matatizo makubwa ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria huku wanaume wakiwakana.

"Asilimia kubwa ya dawa tulizozikamata tumezikuta zikiwa kwa wanawake una mkuta mtu mmoja anawanawake zaidi ya wawili mpaka watatu na kuficha dawa za kulevya katika makazi yao huku wao wakipanga nyumba tofauti wanakoishi wapenzi wao" amesema Kamshina Jenerali Lymo.

"Kifungu cha 15 cha sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya kinaeleza kwamba ni kosa kusafirisha dawa za kulevya na mtu yoyote atakayethibitika kutenda kosa atawajibishwa kisheria"amesema Kamshina Jenerali Lymo.

Hata hivyo, amesema Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha inamaliza tatizo la dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii kutokana na kuwepo kwa madhara makubwa ya kiuchumi na kijamii .

Aidha, amesema kuwa operesheni maalumu ya kukamata na kudhibiti dawa za kulevya iliyofanyika katika mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Kilimanjaro na Pwani ambayo imefanikiwa kukamata dawa mbalimbali za kulevya na watuhumiwa wa biashara hiyo.

Katika hatua nyengine kupitia Operesheni hiyo  DCEA imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5, bagi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5465, bagi iliyosindikwa kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3878, cocaine kete 138 , mililita 3840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1093 za mashamba ya bangi.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...