ONESHO LA KWANZA LA EONII JUNE 23, MLIMANI CITY

 

Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar 

Kampuni ya Azam Media Ltd (AML) kwa kushirikiana na Studio za PowerBrush (PBS) wanatarajia kuonesha  rasmi filamu ya Kisayansi ya EONII Juni 23, 2023 katika Ukumbi wa Century Sinemax Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Azam Media, Divisheni ya Maudhui na Utangazaji Yahya Mohamed amesema mipango yote muhimu imekamilika tayari kwa Onyesho hilo  la kwanza la uzinduzi wa kihistoria.

"Tutumie fursa hii kwa niaba ya Azam Media Ltd na PowerBrush Studios kutambua mchango makubwa wa Serikali yetu katika kusimamia michezo na sanaa nchini na kuweka mipango endelevu ambayo tunashuhudia matunda yake kupitia mageuzi haya kwenye tasnia ya Filamu nchini,"amesema Mohamed.

Aidha, amesema kuwa bodi ya Filamu wamekuwa mhimili mkubwa katika kutoa hamasa, kuratibu njia sahihi za kuisukuma sanaa ya Filamu na kipekee amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka chachu iliyopeleka saa sasa ya Filamu Kimataifa.

Ameongeza kuwa, hamasa hizo na sera na kanuni madhubuti timu yao ya uzalishaji pamoja na PowerBrush Studios wamewekeza katika ubunifu na umakini mkubwa kunadaa Filamu ya EONII ambayo inasukuma mipaka ya kuwaza na kusimulia hadithi.

Amesema juhudi hizo za kipekee ni uthibitisho wa kukua kwa vipaji na matamanio ndani ya Tasnia ya Filamu Tanzania

"Nimatarajio yetu viongozi na waalikwa wengine watakuwa mabalozi Wazuri baada ya onyesho la Awali la Premier siku ya Ijumaa Juni 23, 2023 pale Mlimani City, mabali na onyesho kuu la Dar es Salaam, EONII itaoneshwa katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Tanga na Mwanza kwa upande wa Tanzania Bara, huku Zanzibar ikiwa kituo muhimu," ameeleza Mohamed.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji bodi ya filamu Dkt Kiagho Kilonzo amesema Filamu hiyo ni ya kwanza ilitumia muda wa miaka minne na kugharimu dola laki mbili ikiwa imebeba maudhui ya uhitaji wa nishati ambapo nchi ikiwa katikati ya Ombwe la kukosekana kwa nishati ndiyo filamu inakuja. 

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI