REMBO AKABIDHI PIKIPIKI NA TOFALI 1000 IRINGA

 

Na Mwandishi wetu, HPMedia, Iringa

Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Iringa Injinia Fatma Rembo ambaye pia ni njumbe wa kamati ya utekelezaji wa UWT Taifa, leo amekabidhi pikipiki nne kwenye wilaya za mkoa wa Iringa ili kusukuma maendeleo.

Hatu hiyo imekuja mara baada ya kufanya ziara katika wilaya za mkoa wa Iringa ambapo pamoja na mambo mengine pia amekabidhi Shilingi 1,000,000 kwa wilaya nne  kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za makatibu wa jumuiya hiyo.

Akizungumza na wanachama wa UWT Mkoani humo, wakati wa kukabidhi pikipiki pamoja na fedha kwa ajili ya matofali amesema umoja na mshikamano katika chama chao ndio njia pekee ya kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake katika kumsaidia Rais wa JMT Dkt Samia Suluhu Hassan. 

"Baada ya ziara yangu katika wilaya zote mkoani Iringa  niliahidi kukabidhi pikipiki na fedha kwa ajili ya matofali na leo nimetimiza , hivyo naomba tuendelee kumuunga mkono Rais wetu lwa kumsemea mazuri, pikipiki hizi naomba ikawe chachu ya kusaidia kuzitatua changamoto za kiuchumi" amesema Rembo.

Aidha, amezitaja Wilaya zilizopewa pikipiki hizo ni pamoja na Mufindi, Kilolo, Iringa Mjini na Iringa Vijijini, huku akiwataka wazitunze ili ziendelee kusaidia kazi mbalimbali za uchumi.

Awali akipokea pikipiki hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comred  Daud Yasin Mlowe, amempongeza Injinia Rembo kwa kutoa pikipiki hizo pamoja na fedha huku akisisitiza kila kiongozi kutekeleza wajibu wake ili wananchi waweze kupata maendeleo ya haraka.

"Tuendelee kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii, tuendelee kumsemea na kutangaza mazuri anayoyafanya ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kuvutia wawekezaji" amesema Comred Yassin.

Naye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Comred Salim Asas Abri  alisisitiza upendo, huku akiwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kumtetea Rais wa JMT Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuitangaza nchini ya Tanzania katika mataifa mbalimbali .

"Kina mama naomba mupendane, mkiyumba nyie chama kimeyumba pia, mkiona mwenzio amefanya jema mpongeze, pia muwe mstari wa mbele kumtetea mwanamama mwenzenu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan"amesema Asas.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa, Comred  Zainab Mwamwindi amempongeza Injinia Rembo kwa jambo kubwa alilolifanya katika chama na jamii kiujumla huku akiwataka na viongozi wengine kuiga mfano wake katika kusaidia harakati za kimaendeleo.




Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...