UVCCM TAIFA - "HAWANA HOFU MASHIRIKIANO YA KUIMARISHA UCHUMI WA BANDARI"
Na Magrethy Katengu, HPMedia, Dar
Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umesema Serikali inachofanya sasa ni mashirikiano ya Uwekezaji Bandarini ili kwenda kusaidia kuimarisha miundombinu ya bandari na shughuli nyingine za lojistiki na Uchukuzi ili Taifa liwe kitovu cha uchumi Imara.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Mohamed Kawaida, amesema kinachofanyika siyo maamuzi ya mtu binafsi bali ni maelekezo ya Chama kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kupitia ibara 22(1)
Aidha amesema kuwa, kupitia uwekezaji ambao utafanyika utasaidia kuondoa urasimu na dosari zinazosababisha ucheweshwaji wa utoaji mizigo Bandarini.
Hata hivyo, amesema licha ya kusambaa mizozo mitandaoni kuhusu bandari, katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 (a) inaeleza"kila mtu anao Uhuru wa kuwa na maoni ya kueleza fikra zake "hivyo wanaheshimu maoni ambayo yanatolewa na yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali kuhusu azimio hilo ambalo linaridhiwa na Bunge kwa mujibu ya Ibara 63-3(e) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka Mkataba unaoingiwa na Serikali upitiwe Bungeni kabla ya kutekeleza .
"Serikali ya Tanzania imeingia Mkataba wa mashirikiano na serikali ya Dubai kwa kuanzisha Ushirikiano wa kuboresha ,kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini suala ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa serikali kufikia malengo ya kiuchumi na kijamii na majadiliano haya na maandalizi yanafanywa na Timu ya wataalamu wa Tanzania ambao Wana uzoefu mkubwa katika Masuala ya mikataba ya kinataifa na kabla ya kusainiwa ulizingatia taratibu zote za nchi yetu " amesema Kawaida
Hata hivyo, amebainisha kuwa Ushirikiano pamoja na mambo mengine unajikita kwenye maboresho uendeshaji wa shughuli za bandari nchini kwa kuongeza tija na ufanisi kusimika mfumo ya kisasa ya TEHAMA na kuwajengea uwezo kupitia mafunzo Watanzania katika uendeshaji wa shughuli za bandari kuhusu changamoto za bandari mifumo ya TEHAMA ya bandari kisasa na inayosoma na mifumo mingine ikiwemo Mamlaka ya Mapato TRA hali inayosababisha kutokuwa na udhibiti wa kutosha katika kukusanya mapata ya nchi.
Aidha amesema kuwa jitihada zote na hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya Awamu ya sita katika kuvutia uwekezaji nchini hususani kwenye maeneo ya bandari nchini zinalenga kumalizia changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika bandari zetu ambako kumekuwa kukichangia katika sekta zingine .
Comments
Post a Comment