KUTOKA KWA RAIS DKT SAMIA

 

Juma hili tumekuwa na mkutano na mjadala muhimu baina ya viongozi na wakuu wa nchi za Afrika kwa maendeleo na mustakabali wa nchi zetu na Bara letu, kuhusu Maendeleo ya Rasilimali Watu.


Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuijalia nchi yetu fursa hii adhimu ya kukutanisha viongozi hawa katika nchi yetu kwa jambo hili lenye kheri na muhimu kwa maendeleo yetu.

Mkutano huu umebeba kaulimbiu ya “Kuchochea Ukuaji wa Uchumi Afrika: Kuongeza Uzalishaji wa Vijana kupitia Mafunzo na Ujuzi’’, ajenda ambayo ndio moyo wa mataifa yetu – uwekezaji katika rasilimali watu, hususani vijana. 

Mbali na kufikia azimio la pamoja (Azimio la Dar es Salaam) ambalo pamoja na mambo mengine litakuza ushirikiano wetu katika uwekezaji na maendeleo ya rasilimali watu, tumeshirikishana yale yanayofanyika katika nchi zetu.

Sisi Tanzania tunaamini katika falsafa za waasisi wetu kuhusu umuhimu wa uwekezaji katika rasilimali watu ili kuleta maendeleo na uhuru wa kweli. Falsafa hizi bado zinaishi na ni sehemu ya dira yetu katika utendaji. Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema, “Maendeleo ni watu. Watu ndio walengwa, waanzilishi na wanufaika wa chochote kinachoitwa maendeleo.”

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...