SERIKALI MBIONI KUZIFUTA KAMPUNI ZILIZOPITWA NA WAKATI

TIPER YATOA GAWIO LA BILL 2.5


Na fatma Ally, HPMedia, Dar 

Serikali inajipanga kuyafuta baadhi ya makampuni ambayo yamepitwa na wakati na kuyaunganisha ambayo yanafanyakazi zinazoshabihiana katika utoaji wa huduma kwa wateja baada ya kufanyika kwa uchambuzi wa kina ambao ritopi yake itakamilka mwezi ujao.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Msaliji wa Hazina Nehemia Mchechu wakati alipokuwa katika hafla ya makabidhiano ya gawio la shill bill 2.5 kutoka kampuni ya Uhifadhi wa Mafuta Tanzania International Petroleum Reserves (TIPER) ambapo amesema lengo la Serikali la kuyaunganisha makampuni hayo ni kuleta tija zaidi.

Aidha amesema kuwa, fedha hizo zilizotolewa na kampuni hiyo zitakwenda kusaidia katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, huku akifafanua kuwa, uchambuzi huo umeshafanyika kwa awamu ya kwanza na unaoendelea sasa hivi ni awamu ya mwisho ambao utakuja na majibu ambayo yatatangazwa baada ripoti ya uchambuzi huo kukamilika.

Aidha, amesema lengo la uwekezaji ni kuona makampuni yakiongezeka katika mchango wa taifa na sio ya kikodi bali kama ilivyofanya kampuni ya Tiper kutoa gawio huku ikiwa imeshatoa kodi zote za Serikali. 

"Kuna timu inaendelea kufanya uchambuzi zaidi na mwezi wa nane ripoti itapelekwa na hapo ndipo itatangazwa ni makampuni gani itaunganishwa au kufutwa kwani kuna baadhi ya kampuni zimekua zikifanya vibaya kutokana na viongozi wake, hivyo wapewe muda wa kuangalia "amesema Mchechu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhifadhi Mafuta Tiper Mohamed Seif Mohamed amesema  wamejipanga kuwekeza zaidi sio tu kwenye uhifadhi wa mafuta bali pia kwenye miundombinu ikiwemo sekta ya usafirishaji, kilimo, bomba pamoja pampu za kusukumia mafuta.

Aidha, amesema kuwa,sekta ya mafuta ni sekta muhimu na nyeti katika nchi yoyote ile duniani na ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na pia kwani ni tegemeo kubwa kwa kila mahali ikiwemo mifumo ya umeme, teknolojia pamoja na rasilimali watu.

Aidha, amesema uwekezaji wao umekua ukifanyika kwa miaka 10 iliyopita na wamekua wakindelea kwani ni jambo endelevu na kufanya hivyo, awamu kwa awamu, hivyo wanawahakikishiawateja wao wapo vizuri katika suala la uhifadhi na utunzaji wa mafuta, ambapo mpaka sasa kuna mafuta ambayo yameshalipiwa na mengine yanasubiri kulipiwa ili yatolewe.



Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI