WAZIRI PROF MKENDA AITAKA BODI YA MAKTABA KUEKEZA UNUNUZI WA VITABU.

 

Na Mwandishi wetu,  HPMedia, Dar 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameitaka bodi ya Maktaba kuwekeza zaidi kwenye ununuzi wa vitabu kuliko ujenzi wa majengo ya Maktaba kwani wanaweza kushirikiana na mashule kuanzisha maktaba za jumuiya.

Kauli hiyo ameitoa Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitembelea ukarabati wa bodi ya huduma za maktaba ambapo amesema ni vyema kuwekeza katika ununuzi wa vitabu kuliko kujenga kwani kunachukua gharama sana.

Aidha, amesema kuwa kuna changamoto kubwa ya uandishi na usomaji wa vitabu kutokana na wanaochapisha vitabu kukosa soko ambapo baadhi ya waandishi kutumia pesa zao kugharamia na wengine huacha kabisa.


 "Zamani wakati ninasoma Maktaba zilikuwa nyingi kutokana na kuwekwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kanisani, misikitini na majengo ya Serikali hivyo niishauri bodi kutafuta maeneo ambayo wataweka vitabu ili kizazi cha sasa kuweze kusoma kwani kusubiri ujenzi wa Maktaba itachukua mda na kizazi cha sasa kitakosa kusoma" amesema Prof Mkenda.

Hata hivyo amesema katika kupunguza changamoto ya ukosefu wa sehemu za kuuza vitabu vinavyochapishwa wameanzisha tuzo za uandishi ya Mwalimu Nyerere ambapo mshindi vitabu vyake Serikali itanunu na kusambaza kwenye maktaba na shuleni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Mboni Ruzegea amesema lengo kuu la maktaba ni kutoa fursa kwa umma kujipatia maarifa endelevu kwa watu wote kupitia usomaji wa machapisho mbalimbali.

Hata hivyo, amesema kuwa maktaba ni chombo muhimu na moyo katika taifa hususani kukusanya na kuhifadhi nyaraka kuwapatia walengwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo ambapo Mwal Nyerere alisema vitabu njia nzuri katika kujiendeleza na kujitegemea.

Aidha, ameiomba Serikali kuisaidia  taasisi hiyo kwa kuiongezea gari kwa ajili ya kusafirisha vitabu ambavyo vimekuwa vikigharimu gharama kubwa wakituma kupitia shirika la posta pamoja na gari kwa ajili ya huduma za chuo.

Aidha, amesema maktaba inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa fedha, Changamoto katika chuo na maktaba ambazo zipo mikoani zinazohitaji ukarabati, uhaba wa vitendea kazi na vitabu vya kiada.




Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI