IGP WAMBURA ATOA ONYO KWA WANAOTISHIA KUIANGUSHA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

 

Na Mwandishiwetu, HPMedia, Dar

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camilius Wambura ametoa onyo kali kwa  kundi la watu waliosambaza taarifa kuwa  wanaandaa maandamano nchi nzima juu ya kuiangusha Serikali ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025, kwani Jeshi la Polisi halitakaa kimya na kuwavumilia kitendo wanachotaka kukifanya cha kuvunja amani iliyopo. 

Onyo hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuna watu ambao wanasambaza taarifa za ajabu huku zikihusisha maaandano nchi nzima, huku wakiwashawishi watanzania wawaunge mkono katika hoja zao.

Amesema kuwa, maandamano hayo wanayoyapanga kushawishi jumuiya ya watanzania na kuwataka waunge mkono mjadala wa Bandari unaoendelea.

"Sisi tuliamini suala la bandari linajibiwa kwa hoja na na vilevile tukaamini kwa sababu hawa watu walikwenda mahakamani wangeheshimu maamuzi ya mahakama lakini badala yake wametoka Sasa na kuanza kutafuta ushawishi na kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima na miongoni mwao mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaangusha Serikali ya jamuhuri ya muungano ya awamu ya sita"amesema IGP Wambura

IGP Wambura amewataka wasitishe kabisa matamshi yao ya kichochezi watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa uhaini wanaotaka kuufanya kwani yote ni makosa ya jinai.

" Kama munafikiria tuko kimya tuko basi tutakwenda kuwaonyesha hatuko kimya kwa yeyote anayevunja sheria ya nchi hivyo niwatake watanzania wawapuuze watu hawa kwani Tanzania ni Nchi ya amani na Salama hawa wasitake kuwashawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko hatujawahi kufika huko na hatutofika kwenye machafuko " Amesema IGP

Aidha amesema kuwa, wachochezi hao wanatakiwa kutambua kuwa Jeshi la polisi ni imara sana wasitikise kiberiti kama wamewahi miaka ya huko nyuma na wakaguswa wasithubutu kwenda hatua nyingine huko wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya sana hivyo wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na kufanya shughuli zao za kiuchumi kama ilivyokuwa desturi yao.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...