MAENDELEO BENKI YAADHIMISHA MIAKA 10 KWA MBIO ZA HISANI



Na fatma Ally, HPMedia, Dar

Katika kusherehekea kutimiza miaka 10 ya benki ya Maendeleo imeandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kukusanya shill mill 200 ambazo zitakwenda kusaidia vituo viwili, ikiwemo kituo cha KCMC kilichopo kilimanjaro na Kituo cha kulea watoto wenye chamgamoto ya afya ya akili kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa matembezi hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema ili kufikia upatikanaji wa fedha hizo ni lazima washiki wote katika matembezi hayo wafikirie upatikanaji wa fedha hizo ikiwemo kununua begi linalouzwa lenye vifaa mbalimbali .

"Katika kuunga mkono zoezi hili nakuomba DAS ilala uchukue begi 10 ikiwa ni sehemu ya uchangiaji wetu Halmashauri ya ilala, niwaombe pia wadau wote tuchangie hizo fedha isiishie tu kutembea hadi viwanja vya farasi bali tuhitimishe kwa upatikanaji wa hizo mill 200"amesema DC Mpogolo.

Ameongeza kuwa, wanatafuta fedha hizo lwa ajili ya watoto wenye usonji aweze kujengewa ukuta, kuboreshewa madarasa , kutengenezewa vitanda hiyo ikimaanisha kama mtu ana mashuka mazuri apeleke, ndoo za rangi, pamoja na tofali.

Sambamba na hayo amesema wanatafuta vitanda na vifaa tiba kwa ajili ya kituo cha KCMC kwani kituo hicho hakihudumii tu watu wa kilimanjaro bali kinahudumia akina mama wajawazito wanapopata matatizo, wafikirieni watoto njiti hizo ndio kilomita sita zinazotakiwa kutembewa.

Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesemq ameipongeza benki hiyo kwa hatu ya kuishirikisha jamii kwani benki nyingi zinaangalia faida, ambapo miaka ya zamani watotk hao walikua hawana nafasi ya kuwa hai lakini benki hiyo imewafikiria watoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo benki Dk Ibrahim mwangalaba amesema kuwa, benki hiyo imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ikiwa imefikisha jumla ya mali shill bill 114 na amana shill bill 81 ambapo wametoa mikopo kwa wateja mbalimbali sasahivi zaidi ya shill bill 66 ambapo wametoa na kurudisha shill bill 400.

Amesema kuwa, benki hiyo imechangia ajira kwa watanzania mbalimbali ukizingatia benki ilianzishwa ikiwa watumishi 13 na sasa wamefikia 114 ambapo ya mwaja huu kumalizika wataanzisha huduma ya internet banking huduma ya kimtandao.



Aidha, amesema kuwa benki imeamua kuchukua hatua ya kukabiliana na changamoto za afya ya mtoto kupitia ushirikishwaji wa jamii hivyo katika kusherehekea miaka 10 wameandaa mbio za hisani zenye kauli mbiu za hatua za faraja, ambapo mbio hizo zinadhumuni ya kuhama watu mbalimbali ambapo fedha hizo zitatumika kusaidia vituo viwili vyenye mahitaji maalum.


Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI