MAWAZIRI, WANASHERIA WAJIFUNGIA DAR KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Na fatma Ally, HPMedia, Dar
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amesema kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watanzania hawaifahamu katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo wengine hawajaiona kabisa hivyo ni wajibu wao kuhakikisha watanzania wanaifahamu ili kupuuza maneno wanayoambiwa.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akifungua kikao cha Mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu wa Serikali wastafu na waliopo madarakani kuhusu majadiliano ya mchakato wa katiba mpya pamoja na mkakati wa Taifa wa elimu ya umma (MTEKU 2023/2026).
Amesema kuwa,ipo haja ya watanzania kueleweshwa kuhusu katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuijua ili kuuza maneno wanayoambiwa ambayo hayahusu katiba ikiwemo kupanda kwa bei bidhaa ikiwemo vyakula pamoja ugumu wa maisha.
"Wapo watanzania ambao hawaijui kabisa katiba na wengine hawajaiona kabisa hivyo ni muhimu kuifahamu ili yanapozungumzwa mambo yanayohusu katiba iwe ni rahisi kuweza kuyafahamu kwa upana wake, ili wasije wakaingiziwa mambo ambayo siyo ya kikatiba"amesema Dkt Ndumbaro.
Ameongeza kuwa, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa siasa wamekua wakijadili sana kuhusu mchakato wa katiba mpya ambapo wengine wanatofautiana katika mitazamo yao juu ya mchakato wa katiba mpya.
"Wapo ambao wanataka mchakato uishie ulipoanzia, wapo ambao wanataka twende kwenye rasimu na wapo ambao wanataka sheria zibadilishwe, leo tutayapitia maoni yote ili tutoke na kauli ya pamoja kuhusu katiba mpya"amesema Waziri Dkt Ndubaro.
Aidha, amesema kikao hiko kitapokea maoni ya mchakato wa katiba mpya kutoka upande wa Tanzania bara na Zanzibar ili kufahamu ni maeneo gani ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho katika katiba ya mwaka 1977.
Kwa upande wake, Waziri Mstaafu wa Katiba na Sheria Mery Nagu amesema ujio wa katiba ni muhimu sana kwa Taifa hasa linalopiga hatua kiuchumi na kisiasa kwani kuna baadhi ya vifungu vya sheria vilivyopo kwenye katiba ya 1977 vinahitaji vifanyiwe marekebisho.
Comments
Post a Comment