TANZANIA KUJENGA USHIRIKIANO NA INDIA MAONYESHO YA CHAKULA



Na fatma Ally, HPMedia 

Tanzania kwa kushirikiana na India kupitia mkutano wa kimataifa wa chakula ambao unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika wataweza kukabiliana na changamoto zilizopo na kuimarisha zaidi mahusiano yao na kuongeza uwekezaji kutoka India ambao utaongeza pato la taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TASO Event Suveer Rajpuexlint amesema kwani India ni soko kubwa kwa nchi za Afrika hivyo Afrika wanakaribishwa kuwekeza nchini humo.

Aidha, kupitia mkutano huo utajenga ushirikiano kati ya India na nchi za Afrika kwenye maswali ya kiuchumi kibiashara na kijamii.

"Mahusiano kati ya Afrika na India yanazidi kukua hususani sekta ya kilimo kwani changamoto za wakulima Afrika zinafanana na za India hivyo lengo lao ni kukuza wakulima wadogo na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na India kwenye bidhaa za kilimo"amesema.

Aidha, amesema Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Chakula ambao kwa mara ya kwanza unafanyika Barani Afrika ukihusisha kampuni 500 toka nchini India na Asia katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Amesema teknolojia pia inasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo zile za mabadiliko ya hali ya hewa, na uhaba wa maji hivyo wakishirikuana kwa pamoja na kutatua changamoto wataweza kuzalisha bidhaa na kuilisha Afrika na Asia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Pulses Network (TPN) Lirack Andrew amesema dhima ya mkutano huo ni kufungua masoko kwa mazao ya Afrika na kutoa taarifa kwa duniani nzima kuhusu uzalishaji uliopo Afrika ili nchi zenye uhitaji zifahamu na kuagiza bidhaa kutoka Afrika.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika maonyesho hayo ambayo yatawawezesha kujenga mahusiano na kampuni za nje zitakazoshiriki kwenye maonyesho hayo na kukuza teknolojia zao na kupata fursa za masoko ya bidhaa zao.

Aidha amesema kupitia maonyesho yatakayofanyika wanatarajia kupokea watu zaidi ya 3000 ambao watatembelea mabanda ya wafanyabiashara na makampuni hivyo kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana uzoefu.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI