WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KILIMO
Na Mwandishiwetu, HPMedia, Dar
Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRED Latifa Khamis amezindua kongamano la kimataifa la biashara ya mazao ya kilimo (World agrifam) ilikua lengo kuu ni kufungua fursa kwa wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde korosho mafuta pamoja na pamba kwa kwani walaji wakubwa wa mazao hayo ni bara la Asia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua kongamano hilo wakati akimuwakilisha Waziri wa Viwanda Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa, ni jambo la kupongezwa kwa ubalozi wa India kwa kuamua kuleta kongamano hilo Nchini Tanzania kwani wakulima wadogo watapata fursa ya kuonana na wahusika wenyewe wanaojihusisha na mazao ya kilimo.
Aidha, amewataka watanzania kushiriki kwa wingi katika kongamano la kimataifa la biashara ya mazao ya kilimo World agrifam ili kuweza kupata fursa ya kuuza mazao mbali mbali nje ya nchi.
Amesema kuwa, kwa mazao ya kilimo yamekuwa yakifanya vizuri katika soko la nje hususani zao la parachichi kutoka mkoa wa mbeya .
"Hatukutegemea kama zao la parachichi kutoka mbeya lingeweza kufanya vizuri lakini tumeskia namna ambavyo linavyofakazi hivyo ni waombe wakulima wazidi kujitokeza ili kuweza kupata uzoefu wa kilimo"amesema Latifa .
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Pulses Network (TPN) Zirack Andrew ambaye pia ni muandaaji wa kongamano hilo amesema mkutano huo wa mazao ya chakula unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika hususan nchini Tanzania.
Amesema kuwa, kongamano hilo limefanikiwa kuleta makampuni zaidi ya 700 kutoka nchi mbali mbali duniani kote na ni kongamano ambalo linajumuisha mazao yote yanayolimwa afrika.
Aidha, amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni sekta ya chakula Bora kwa ajili ya ustawi wa afrika ambapo wamewakutanisha wanunuzi kutoka nje na wauzaji wa ndani ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na uwekezaji katika ongezeko la thamani .
"Bado Teknolojia yetu sio nzuri kitu ambacho mazao yetu ya chakula huuzwa chini ya kiwango hali inayopelekea bei ya chakula kuwa chini wakati tungeweza kuchakata chakula tungeweza kuuza katika thamani ya juu"amesema Andrew.
Hata hivyo, amewataka watanzania ambao bado hawakuweza kufika katika kongamano hilo ni vyema kufika katika viwanja hivyo vya diamond jublee ili waweze kujifunza vitu mbali mbali.
Amesema kongamano hili limeanza Jana hadi Agost 12 ambapo yatahusisha wataalam kutoka nchini India na makundi ya wakulima wa Bara la Afrika, ambapo zaidi ya watu 3000 watembelea na kushiriki maonesho haya, dhamira ni kufungua masoko ya Mazao yetu ya chakula ya Afrika Kimataifa.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer, Suveer Rajpurohit, amesema kwamba wamekuja barani Afrika kwa ajili ya kutafiti fursa ya soko kwa mazao ya Kilimo ya Afrika na India,huku akiwakaribisha wakulima kutembelea maonesho hayo ili kuona fursa mbalimbali zitokanazo na Kilimo.
Comments
Post a Comment