ZUNGU ATOA MAJIKO YA GESI 200 KWA MAMA LISHE ILALA

 

Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amegawa majiko 200 ya gesi kwa mama lishe wa soko la Machinga Complex lililopo Ilala Ili watumie nishati mbadala waache kutumia kuni katika kupika chakula .

Akizungumza mbele ya mama lishe hao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema Rais wa Dkt Samia Suluhu Hassan anajali afya za wafanyabiashara  wa mama lishe ndio maana amewagawia majiko Ili kurahisisha mapishi waache kutumia mapishi ya kutumia moshi ni hatari katika afya .

"Tumegawa majiko ya gesi kwa mama lishe wa Ilala soko la Machinga Complex, Ilala Boma, Mchikichini na Gerezani, hii itawasaidia mama lishe kupika chakula na kupasha moto kila wakati kwa wateja wao itawavutia biashara zao "amesema Zungu .

Aidha, amewataka waondokane na kasumba kwamba chakula ukipika na gesi sio kizuri badala yake watumie gesi katika mapishi yao mapishi ya gesi hayana  moshi na chakula kinakuwa kisafi .

Amesema kuwa, mapishi ya mama lishe wakitumia gesi inaokoa pesa kwa kutumia nishati mbadala pia hawawezi kupata ugonjwa wa kifua kikuu .

Ameongeza kuwa, hewa ya ukaa inaenda angani kuharibu mazingira majiko ya gesi watu watakuwa salama bila kupata magonjwa na nazingira hayawezi kuharibika .

Kwa upande wake, Meneja wa Soko la Machinga Complex Stella Mgumia, ameipongeza Serikali kupitia Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, kugawa majiko ya gesi kwa mama Lishe wa Machinga Complex .

Aidha Meneja huyo  amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo ambayo sio rasmi kuondoka maeneo hayo kwenda kufanya biashara zao Machinga Complex na wauza chips na mihogo waliopo pembeni mwa barabara ya Kawawa waondoke maeneo hayo .

Aliwataka wafanyabiashara kufanya biashara zao katika soko la Machinga complex kwani kuna fursa mbalimbali za kukuza uchumi .

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...