KAMPUNI TANO ZA WAZAWA ZASHINDA ZABUNI UCHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE
Na Fatma Ally,HPMedi, Dar
Katika kuhakikisha Serikali inatoa kipaumbele kwa wawekezaji wazawa imetiliana saini na kampuni tano za kitanzania ambazo zimeshinda zabuni ya uchimbaji wa makaa ya mawe eneo la Mchuchuma Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mchimbaji na Mwekezaji wa Madini kutoka kampuni ya Cleveland Minging and Cervice Compan, Ndaisaba George Luhoro amesema kwa sasa wanaenda kuandika historia na kuongeza ajira katika pato la taifa kwa makaa ya mawe waliyokuwa wanayasikia toka wazaliwe sasa wanaenda kuyachimba.
"Kampuni yangu pamoja na makampuni mengine tulikuwa kwenye ushindani mkubwa ila kwa bahati nzuri kampuni tano ikiwemo na ya kwangu tumefanikiwa kupata mkataba huu hivyo tunaenda kuandika historia yale makaa ya mawe toka tuzaliwe tulikuwa tunayasikia sasa tunaenda kuya chimba na kuongeza ajira Kwa watanzania na kuchangia uchumi Kwa nchi yetu"amesema Mwekezaji Luhoro.
Aidha, amesema kupitia uchimbaji huo wataongeza pato la nchi kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali hivyo anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaonyesha watanzania mapenzi ya dhati.
Ameongeza kuwa, kutokana na uhitaji wa makaa hayo ndani na nje ya nchi watahakikisha wanazalisha kwa kiwango kikubwa zaidi ili kuhakikisha wanafikia malengo ndani ya muda ambao umepangwa.
"Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema makaa ya mawe haya yakachimbwe na watanzania na sisi ni mashuhuda wa mapenzi yake ya dhati sasa tunaenda kuyachimba haya makaa ya mawe na kunufaisha taifa letu"ameongeza Mwekezaji Luhoro.
Hata hivyo, amesema wamepewa mda wa miezi sita kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu zote na kuanzia uchimbaji wa makaa ya mawe na kuanzia kuzalisha angalau kwa mwezi mmoja wazalishe tani laki moja na nusu kwani kwa sasa yanahitajika sana Dunia hasa kipindi hiki ambacho Dunia inapambana kupata nishati.
Aidha amesema matarajio yao ni kukuza kampuni zao na kutoa ajira na kuchangia kwenye pato la taifa na kampuni zao kuzidi kukuza na kuchangamkia fursa za uchimbaji wa madini mengine hata nje ya nchi kwani mkataba huo unaenda kuwa mtaji mkubwa kwenye kampuni zao na kukuza ujuzi kwenye uchimbaji.
Comments
Post a Comment