TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO YAIGUSA JAMII


Na Mwandishi wetu,HPMedia, Dar

Katika kuhamasisha elimu nchini Tanzania, Taasisi ya mama ongea na mwanao imelenga kufanya kampeni ya kugawa viatu kwa watoto mashuleni (wanafunzi) hususani vijijini nchi nzima lengo ni kuwaenua watoto hao kutokatisha ndoto zao za masomo.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Steven Mengele amesema lengo la kampeni hiyo kuinga mkono Serikali katika kuisaidia jamii ambapo zoezi hilo wanatarajia kuanza mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

"Zoezi hili tutalifanya nchi nzima tumelenga vijijini na tutalifanya wenyewe na si kukabidhi kwa uongozi wa shule kwani lengo letu ni kuhakikisha viatu hivi vinamfikia mlengwa moja kwa moja"amesema Steve.

Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka miundombinu mizuri katika sekta ya elimu hivyo wanawajibu kama taasisi inayounga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt Samia kuhakikisha watoto wanaipenda shule.

"Miundombinu imeboreshwa sana, sasa tunataka huyu mtoto aipende shule watoto wengi vijijini wamekuwa wakienda shule peku au na malapa hii hali inapelekea mtoto akichomwa tu na miba njiani kesho hataki tena kurudi shule,"amesema Mengele

Hata hivyo, ametoa wito kwa viongozi wote wa mikoa watakayopita  kutoa ushirikiano kwa taasidi hiyo  ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kama ambavyo wamekusudia katiks kuisaidia jamii.

Kampeni hiyo ilianza mwaka Jana ambapo waligawa zaidi ya viatu 2000 Kwa watoto katika mkoa ya pwani wilaya ya Kibiti na mkoa wa Tabora na wilaya zake.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI