WATANZANIA WATAKIWA KUFANYA MAOMBI


Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar

Nabii wa Taifa Dkt. Kennedy Mwasumbi kupitia huduma ya Tanzania Itubu Ministry amesema kutokana na mambo yanayoendelea kwa sasa, Tanzania hali sio nzuri, hivyo kuna haja kama taifa kufanya maombi ya kutubu.

Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amekua akipata maono kuhusu nchi ya Tanzania, hivyo anaomba kuonana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwenda kumueleza kwa mustakabali wa nchi.

"Nimejitokeza mbele yenu waandishinwa habari kuongea na watanzania kupitia vyombo vyenu, watanzania wanatakiwa wafanye maombi ya kutubu ili nchi iwe salama ipate utulivu, nchi yetu sio maskini lakini inahitajika kufunguliwa macho ili kuufikia utajiri uliopo,lazima tumtegemee Mungu"amesema Nabii Mwasumbi.

Hata hivyo, amesema kumekuwa na mijadala mingi kupitia makundi tofauti kutumia sheria kutafsiri mambo kupitia hiyo mijadala kuna wenye hila wanaojificha nyuma ya matukio hayo hivyo ili nchi iendelee kuwa na amani na Rais Dkt Samia atawale vizuri na makanisa yaendeshwe vizuri lazima kuchukuliwe hatua ya maombi na kutubu.

"Jambo ambalo nataka kwenda kuzungumza na linamsaada kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge letu, vyama vya siasa na vyombo mbalimbali hususani vya dini ikiwemo TEC na CCT na nimepata ujasiri wa kuja kuzungumza kwa sababu mwaka 1997 na mwaka 2015 Mungu amekuwa akinisemesha vituo vinavyohusiana na nchi hivyo nikipata nafasi ya kuonana na Rais nitamueleza kwa manufaa ya nchi yetu"amesema Nabii Mwasumbi.

Aidha amesema katika unabii aliotoa ni pamoja na  kusema kuwa nchi ya Tanzania sio maskini ila tatizo liko kwenye ufahamu na kufunguliwa macho kuwa wakimtegemea Mungu Tanzania ni tajiri.

"Hapa tulipofika hali ya nchi sio nzuri, tunatakiwa kumuomba Mungu ili neema itokee, unapozungumza nchi ni habari ya watanzania wote kwa ujumla ambao wanahitaji kupata mema na utulivu wa kutosha sasa kama utulivu ukikosekana hakuna kitu kizuri kinaweza kutokea na watu wakafurahi lakini mabaya yakitokea ni hatari na mbaya sana"ameongeza Nabii Mwasumbi.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Pentekoste PCCT Tegeta Dkt. Fredrick Simon amewaomba watanzania kuwa na wakati mzuri wa kumuomba Mungu na wanatarajia kuwa Dodoma kuanzia tarehe 27 hadi 30 mwezi mwezi wa 9/2023 kwa ajili ya kuliombea Taifa.

Amesema kuwa, taifa linahitaji maombi na bila msaada wa Mungu haliwezi kusogea na kufika mbali hivyo watanzania wajitokeza kwa wingi Dodoma katika ukumbi wa African Dreams Conference Center ambapo maombi ya kuliombea Taifa yatafanyika.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI