NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar
Mfuko wa Bima wa Taifa wa NHIF imefanya maboresho ya kitita cha mafao kwa wanachama wake ambayo utekelezaji wake utaanza rasmi Machi Mosi mwaka 2024 ikwa lengo ni upatikanaji wa huduma bora wa wanachama pamoja na kuongeza huduma ambazo hazikuepo hapo awali.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt Bernad Konga amesema maboresho ya mwisho ya kiticha cha mafao ya mfuko huo kichotumika sasa yalifanyika June 2016 sawa na takribani miaka 8 iliyopita na hivyo upo umuhimu wa kufanya marejeo yake kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha, amesema kuwa, maboresho hayo ya orodha ya huduma za matibabu ambazo zinatolewa kwa wanufaika wa NHIF na bei zake ambazo hutumika wakati wa malipo kwa madai ya watoa huduma za matibabu yamezingatia maendeleo ya teknolojia na hali halisi ya bei katika soko pia kuwianisha kitita cha mafao na miongozo ya tiba iliyoboreshwa Ili kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa Kwa wanufaika wa mfuko.
Sambamba na hayo, amefafanua kuwa maeneo yaliofanyiwa mapitio na maboresho ya kitita cha mafao ni pamoja na ada ya usajili na kupata ushauri wa daktari, huduma za dawa, vipimo, upasuaji na gharama za kliniki za kawaida na kibingwa.
"Kuhusu Huduma za dawa jumla ya dawa ya 736 zimefanyiwa mapitio kwa kuzingatia bei ya soko na gharama za uendeshaji na wastani wa faida ,hii itaondoa changamoto ya wananchi kukosa baadhi ya huduma za dawa kutokana na changamoto ya bei, pia tumeongeza dawa mpya 247 ambazo zinatokana na dawa mpya zilizopo kwenye muongozo wa orodha wa dawa muhimu za Taifa (NEMLIT)" amesema Dkt Konga
Ameongeza "Gharama za vipimo 311 na upasuaji zimefanyiwa mapitio kwa kuzingatia bei za soko katika ununuzi wa vifaa na vitendanishi, gharama za uendeshaji na wastani wa faida hii itaondoa changamoto ya kukosekana Huduma za vipimo na upasuaji kutokana na changamoto ya bei"
Hata hivyo, amewaomba wananchi kuendelea kujiunga kutumia na mfuko huo kwani lengo la Serikali ni kutoa huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati, hadi Hospital ngazi ya Taifa.
Aidha, amesema mfuko huo utaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau na itaendelea kuwajulisha pindi maboresho yoyote yatakapotokea Ili kuwa na ufanisi katika utoaji wa huduma huku akiwataka wanachama na watoa huduma watakao pata changamoto wakati wa kutoa huduma kuwasiliana na mfuko huo kupitia kituo cha huduma Kwa wateja 199 bure.
Comments
Post a Comment