TREN YA MWENDOKASI YAANZA MAJARIBIO DAR - MOR0


Na Mwandishi wetu, HabariPlus,Dar

Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo limeanza safari ya kwanza ya majaribio kwa Treni ya umeme ya Abiria (SGR)  kutoka ofisi zake zilizopo jengo la Tinzanite maeneo ya stetion Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo mapema leo hii Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja kadogosa amesema Usafiri huo wa Treni utatumia umeme wa kawaida kutoka TANESCO na wanatarajia kuanza safari za abiria hivi karibuni.

Aidha amewatoa wasiwasi watanzania wanaodhania kuwa umeme ukikatika utaweza kuleta athari kwa Treni hizo kuwa sio kweli umeme wake umeunganishwa kutoka grid ya taifa hivyo si rahisi umeme kukatika kwenye njia ya Treni.

Ameongeza kuwa,katika majaribio hayo walimeambatana pamoja na msemaji wa Serikali, wasanii, waandishi wa habari, wahariri na baadhi ya wafanyakazi wa TRC, ambapo treni hiyo inauwezo wa kutembea Km/h100-160.

Kwa upande wake, Msamaji Mkuu wa Serikali Mohbare Matinyi amesema kuwa, ujio wa treni hiyo ya mwendokasi utakua fursa kwa wananchi ambapo watu wa morogoro na kupeleka Dar es Salaam ambapo zoezi hilo litafanyika kwa mikoa yote ambayo itapitiwa na mradi huo.

"Leo tumeweza kuanza hatua ya majaribio kwa treni yetu ya abiria kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, miezi michache ijayo treni hii itaanza safari zake hadi kufika Dodoma ni jambo la kupongeza kwa Serikali yetu, hii inatoa fursa za kiuchumi wananchi wetu wanatakiwa wafanye biashara na mrandi huu utakapokamilika tutaweza kufanya biashara na nchi jirani"

Ameongeza kuwa "Tren ni usafiri wa usalama na uhakika na wa bei nafuu, hapa biashara zitafanyika wananchi watafaika kwa kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kwa mfano Mkoa wa Dar es Salaam sio wakulima kwa iyo watachukua mazao kutoka Morogoro, Morogoro wataletewa bidhaa za kiwandani kutoka Dar es Salaam ambapo zoezi hilo litafanyika pia na kwa mikoa mengine mradi ukikamilika"amesema Martin.

Imeondoka saa 10:30 asubuhi katika ofisi zake za Tanzanite jijini Dar es Salaam na kufika Morogoro na 12:47 ambapo imefanya tena safari ya kurudi Dar kutoka Morogoro 1:47 .

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI