DC ILALA AIPONGEZA ACB KWA KUFUTURISHA WATEJA, WAFANYAKAZI NA WADAU WA MBALI MBALI.

 


Na Mwandishibwetu

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameipongeza  Akiba Commercial Benk (ACB) kwa kuandaa hafla ya kufuturisha wateja, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo.

 Aidha hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena tarehe 25 Machi, 2024, akiongea katika hafla hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo  ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi,huku akiipongeza benki kwa jambo hilo.

Mpogolo amesema kwamba “kitendo cha kufuturisha kilichofanywa na ACB  ni ibada  ambayo mwanadamu  aliyetunukiwa zaidi anatoa kwa wengine na atapata thawabu kwa kufanya hivyo”.

Aidha, ameipongeza ACB kwa kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania na kuahidi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwa karibu na taasisi za fedha hususan benki ya Akiba katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI