MAMA ONGEA NA MWANAO KUFANYA TAMASHA KUBWA, MIAKA 3 YA RAIS SAMIA NEEMA TUPU
Na Mwandishi wetu, HabarPlus, Dar
TASISI ya Mama Ongea na Mwanao inatarajia kufanya Tamasha kubwa la walemavu ambalo limelenga kuwasilikiza changamoto zao na kuwapatia mahitaji yao muhimu ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluh Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taadisi hiyo, Steven Nyerere amesema kuwa tamasha hilo litafanyika nchi nzima ambapo wataungana na watu wa makundi mbalimbali ikiwemo vijana, mabodaboda, wajasiri amali ambapo kauli mbiu yake "Mtonye Mwenzako Mama Tena".
Amesema kuwa, moja ya mikakati ya taasisi hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo wamekua wakisaidia watu wenye mahitaji maalum ikiwemo kugawa viatu kwa wanafunzi mashuleni.
"Katika miaka mitatu ya Rais Dkt Samia amefanya kazi kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi ikiwemo umeme, sisi kama Taasisi tunawaahidi tutaendelea kuwashika mkondo nyinyi ni wapiga kura nchi hii, nyinyi ni watu kama watu wengine na mnahaki sawa na wengine".
Aidha, amesema Rais Samia amekuwa akijikita katika kusaidia watanzania wa hali ya chini katika kipindi cha miaka mitatu yake ya uongozi anastahili kupongezwa, ameona tatizo la umeme na kulitafutia ufumbuzi na kujenga bwawa la mwalimu nyerere ambalo likianza kutoa huduma tutauza umeme mpaka nje ya Tanzania".
Hata hivyo, amesema pia kwenye sekta ya michezo Tanzania inafanya vizuri imeacha kuwa mtazamaji na mshiriki bali sasa imekuwa mshindani mkubwa na hata kushinda kwenye majukwaa makubwa ambapo wanamichezo wa sarakasi Ramadhani brothers na wengi wengi.
"Na sisi kutokana na jitihada za mama anazozifanya katika kuketa maendeleo katika taifa hili tukajitwika jukumu la kuwavika viatu watoto wa shule ambao hawana uwezo sasa hivi tumebakisha mikoa 13 kukamilisha mikoa yote Tanzania.
Aidha Steve Nyerere amekemea wanaharajati wanaotumia Mitandao ya kijamii kutukana viongozi wa juu Serikalini na kubeza jitihada zao na kuwasisitiza kuwa watumie hoja kupinga na si kutumia matusi katika kukosoa kwao.
Kwa upande wake, Susan Lewis maarufu kama Mama Natasha amesema Taasisi ya Mama ongea na Mwanao inasimamia wasanii mbalimbali ambao wanalenga kutumia Taasisi hiyo kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kusaidia vifaa vya shule vua watoto na kadhalika.
Nae, Katibu wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuwashurikisha mara kwa mara watu wenye ulemavu katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo makongamano, mikutano na warsha ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada watu wenye ulemavu.
"Wanayotafanya mama ongea na mwanao ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu katika adhima yake ya kuwainua watu wasiojiweza, wenye ulemavu,wajasiliamali".
Comments
Post a Comment