ACT YATOA USHAURI KITENGO CHA MAAFA, MAFURIKO RUFIJI GUMZO

Na Mwandishi wetu

IMEBAINISHWA kuwa kuwepo kwa matukio ya majanga kwa miaka mingi ya hivi karibuni imeonesha uwezo mdogo wa kukabiliana na majanga pamoja na kuchukua tahadhari za majanga mbalimbali ikiwemo ajali na moto kutoka kitengo cha maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita amesema kuwa mwishoni mwa mwaka 2023 hadi sasa kumekua na udhaifu mkubwa wa kitengo cha maafa katika kuchukua hatua za dharura pindi majanga yanapotokea.

"Kwa mfano Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitabiri nchi kupokea mvua kubwa lakini watanzania hatukuona hatua madhubuti zikichukuliwa kujiandaa na kujilinda na janga hili ili kuepusha au kupunguza athari zinazowapata wananchi sasa"amesema Waziri Mkuu Kivuli Mchinjita.

Aidha, amesema kuwa, ukanda wa Kibiti Rufiji eneo linalozunguka bonde la mto Rujifi hasa liliopo karibu na bwawa la kuzalisha umeme la Mwalim Nyerere kuna hali mbaya sana, kata zaidi ya 12 zimeathirika vibaya na maji, mazao, makazi huduma msingi za kijamii zimeharibiwa vibaya wananchi wengi wamejihifadhi kwenye shule ambazo hazijapatwa na maji.

Hata hivyo, amesema kuwa kwenye hotuba iliyosomwa na Waziri Mkuu bungeni haijaonesha hatua za makusudi za kujenga uwezo wa kibajeti kununua vifaa vya kisasa vya uokoaji pamoja na kuijengea uwezo idara ya maafa na taasisi zilizochini yake.

Sambamba na hayo Act wameitaka Serikali kuchukua hatua, kutenga bajeti ya kutosha ili kujenga uwezo wa idara ya maafa na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa idara hiyo, ikiwemo kutumia teknolojia ya juu ya kufuatilia maafa sehemu mbalimbali za nchi.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI