TAKUKURU KINONDONI YAPOKEA MALALAMIKO 84, YABAINI MAPUNGUFU MIRADI 6



Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar

Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imebaini mapungufu kwenye miradi 6 ya maendeleo yenye thamani ya bill 61.910.746.284.42 ambapo wameahidi kuifuatilia kwa ukaribu zaidi miradi hiyo ili ikamilike kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni Elizabeth Mokiwa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia January hadi March 2024 ambapo imekua  na utaratibu wa kutoa taarifa ya utendaji kazi kila baada ya miezi 3.

Amesema kuwa, miongoni mwa miradi walioifuatilia ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa michezo Mwenge wenye thamani ya shill 4.065.100.285.23 ambapo umekamilika kwa asilimia 92  huku ikibaki ubandikaji wa kapeti ya nyasi.

"Mradi huu unakaribia kukamilika April 21 2024 kwa mujibu wa makubaliano mkataba, ufuatiliaji wa karibu unaendelea kuhakikisha mradi unakamilika kwa ubora na kuzingatia thamani ya fedha"amesema Mokiwa.

Ameongeza kuwa, pia wamefuatilia mradi wa mikopo wa asilimia 10 kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 katika Manispaa ya Ubungo wenye thamani ta Shill 2.504.217.430.00.

"Fedha, zilizotolewa kwa vikundi 382 ambapo vikundi 281 havijaresha kwa wakati mkopo wa kiasi cha shill 1.448.991.898.00, ufuatiliaji unaendelea ili kuhakikisha fedha za Serikali zinarejeshwa ili kusaidia makundi mengine mengi zaidi kujikwamua kiuchumi"amesema Mokiwa.

Aidha, Takukuru imepokea jumla ya malalamiko 84 ambapo malalamiko 40 yalihusu rushwa na 44 yasiohusu rushwa huku walalamikaji wakishauriwa na majadala kufungwa na wengine wameelekezwa sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao.

"Malalamiko tuliyoyapokelewa Asasi binafsi 35,Tamisemi/Manispaa 19, Mahakama 6, Polisi 7, Benki 5, Elimu 3, Wizara ya ardhi 2, Tlb 1, Dini 1, Jkt 1, Nida 1, Tra 2 pamoja na Dawasa 1 ambapo inafanya jumla ya malalamiko 84 huku malalamiko mengine yalihusu madai, dhulma, kughushi, kutapeli, mikopo umiza na kutoridhishwa na kesi mahakamani"amesema Mokiwa.

Hata hivyo, amesema katika kuhakikisha Takukuru inatoa huduma inayowafikia wananchi wote wamejiwekea mikakati kwa kipindi cha April/Juni 2024 ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Progrumu ya Takukuru-Rafiki kwa lengo la kuendeleza ushirikiano na wananchi pamoja na wadau.

Aidha, amesema wanaendelea kutoa elimu ya rushwa na dawa za kulevya kwa vijana walioko mashuleni ili watambue madhara ya rushwa na dawa za kulevya na kuchukua hatua kwa maslahi ya taifa pamoja na kufanya vikao vya wadau na watoa huduma katika kata zao.

Aidha, wametoa wito kwa wananchi wote katika mkoa wa kinondoni wanapopata taarifa zozote za rushwa  kutoa taarifa kupitia mitandao yote ya simu kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi kwa namba ya dharura 113 bure au uwasiliane kupitia namba ya mkuu wa Takukuru kinondoni 0738150236 pamoja na mkuu wa Takukuru wilaya ya Ubungo 0738150238.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...