HARMONIZE AMPA "ZAWADI" RAIS DKT SAMIA

 

Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar

MSANII wa Bongo Fleva ambae amekua akifanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini,  Harmonize anatarajia kuzindua albam yake ya tano Mei 25, 2024, Jijini Dar es Salaam.

Staa huyo wa muziki wa kizazi kipya amebainisha hayo jana Mei 20 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua kuwa albamu hiyo imebatizwa jina la Mziki wa Samia.

Albamu hiyo imebeba nyimbo 10 za nguvu ambazo zinatangaza mambo mazuri ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uongozi wake.

Mei 25, itakua ni usiku maalum kwa ajili ya watu kuburudika, hakutakya na kiingilio ispokua ni mialiko maalum kwa wageni kuweza kuhudhuria katika hafla hiyo.

Lengo la uzinduzi wa albamu hiyo ni kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

Aidha, album hiyo itakua ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida naametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena.

Amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku wa mialiko na hakutakuwa na viingilio “Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa "Muziki wa Samia"

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI