RAIS DKT SAMIA KESHO KUTUA KOREA, MIKATABA SABA KUSAINIWA
Na Mwandishi wetu, HabariPlus
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku sita nchini korea yenye lengo la kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. anaenda kufanya Ziara ya kikazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba amesema kuwa pamoja na mambo mengine pia atasaini mikataba saba na Rais wa nchi ya korea yenye lengo la ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
"Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na mikataba hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya madini Tanzania na Taasisi ya miamba nchini korea, huu ni ushirikiano unahusu utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na uchoraji wa maabara"amesema Waziri Makamba.
Ameongeza"mkataba wa pili ambao unaenda kusainiwa ni ushirikiano wa uchumi wa bluu, huku mkataba wa tatu ukihusu kwenda kutambua vyeti vya mabaharia na tutaweza kusaini tamko la pamoja kuhusu siasa na makubaliano ya hati ya madini, viwanda na biashara "amesema Waziri makamba
Hata hivyo, mkataba mwingine ni msaada wa fedha kutoka benki ya Exim nchini korea na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao unaenda kupelekea Tanzania kupata msaada na mikopo nafuu, pia wanakwenda kushirikiana na chuo kikuu kutoka nchini korea katika kuendeleza huduma za usafiri wa anga nchini.
Aidha, amesema ziara hiyo imedhamiria kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Korea kwenye mambo muhimu ikiwemo elimu, afya, na miundombinu hivyo ziara hiyo inaenda kuleta mafanikio mbalimbali nchini Tanzania.
Aidha Waziri Makamba ameongeza kuwa kuhusu madini kwenye mkakati watasaini mkataba katika kuwezesha kuchambua, na kufanya mkakati na shirika la madini Tanzania STAMICO na shirika la ukarabati wa madini nchini Korea.
Comments
Post a Comment