TRA YATAMBUA NGUVU DIGITAL PLATFORM


Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA leo imekutana na Jukwaa la wanahabari wa Mtandaoni (JUMIKITA) kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu namna ya utoaji wa elimu ya mlipa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Kaimu Mkurugenzi wa TRA Hudson Kamoga wakati akifungua mafunzo ya siku moja yalioandaliwa na malaka hiyo, amesema TRA imedhamiria kutoa elimu kwa watanzania wote ili waweze kulipa kodi kwa hiari .

Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita imekua na utaratibu maalum wa kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wananchi ili kila mtu atakaponunua bidhaa aweze kudai risiti.

"TRA imekua na utaratibu wa kufuata kodi kwa wafanyabiasha na kutoa elimu ili waweze kulipa kodi bila shuruti, pia tumekua tukifanya ziara ya mlango kwa mlango kwa ajili ya kuskiliza mteja kama anadai risiti na wanafanyabiashara wanatoa risiti hizo" amesema Kamoga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Jukwaa la waandishi wa habari za Mtandaoni, (JUMIKITA) Shaban Matwebe amesema kuwa waandishi wa habariz za mtandaoni wamekua na nguvu kubwa kuweza kuripoti matukio kwa haraka na kuwafikia wananchi wengi.

"Tunaipongeza Serikali kupitia Taasisi hii ya TRA kwa kukutana nasi leo kwa ajili ya kutujengea uwezo, tupate elimu ya ulipaji kodi, nguvu yetu ni kubwa twendeni tukamsaidie Rais Dkt Samia ili wafanyabiasha waweze kulipa kodi kwa hiari"amesema Matwebe.

Aidha, amesema kuwa kwa sasa dunia ipo kiganjani kila jambo lipo mtandaoni hivyo taasisi mbalimbali kutumia jukwaa hilo wataweza kuwafikia wananhi wengi zaidi tena kwa hara zaidi.




Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...