JESHI LA POLISI LAJIPANGA KUKABILIANA NA VITENDO VYA KIHALIFU

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Aprili mwaka huu,limesema limeongeza nguvu ya kukabilli viashiria vya vitendo vya kialifu na waarifu na kufanikiwa kukamata watu 13 wanaotuhumiwa kutumia, kuuza na  kuusambaza dawa za kulevya jijini humo.

Pia kuanzia kipindi hicho limefanikiwa kukamata watuhumiwa hao wakiwa na kete 2,639, misokoto 158 na Puli 531 za bangi iliyokuwa imefungashwa tayari kwa matumizi,  viroba vinne vya dawa hizo pamoja na pikipiki mbili ambazo zinaaminika kutumika kisafirishia.

Hayo yamebanishwa leo, Juni 7, 2024 jijini Dar es Salaam na  Kamanda wa Kanda Maalumu  wa jiji hilo SACP, Jumanne Muliro wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

"Hatutaki kurudi nyuma tulikotoka ambako kulikuwa na vitendo vingi vya kiarifu, tutaendelea kudhibiti viashiria vyote vya kiarifu na waharifu ili  kulifanya Jiji hili kuendelea kuwa tulivu na usalama wakati wote.

"Katika operesheni ambayo tumefanya baada kubaini uwepo wa viashiria vya vitendo vya kiharifu kutaka kufanyika kutokana na baadhi ya watu waliohukumiwa kumaliza adhabu zao na  kurejea  mitaani na kuonekana kutaka kufanya tena uharifu, tumekamata watuhumiwa 13 wakiwa wanapanga njama hovu  wakiwa siraha toi (bandia).

"Katika watuhumiwa hao yupo anayefahamika kwa jina la Hamisi Seif (18) mkazi wa Mbondole na Bosco Bosco mkazi wa Kipunguni Ilala (18), hivyo tunatoa onyo kwa yeyote anayetaka kufanya uharifu afahamu kuwa tutamdhibiti na kumshugulikia kabla hajafanikisha adhima yake na tuomba wananchi waendelee kutupa ushirikiano,"  amesema.

SACP Muliro ametaja pikipiki mbili ambazo zimekamatwa ni MC 673 CKM na MC 591 CUW ambazo zinaaminika zilikuwa zinatumika kusambaza bangi hizo. 

“Jeshi la Polisi linaendelea kusimamia mkakati wakemaalum wa kuzuia vitendo vyote vya kihalifu katika jiji la Dar es Salaam. Kazi hii maalum ya kuzuia vitendo vya kihalifu ni muendelezo wa kazi hiyo iliyoanza Aprili 2024 na inayoendelea kulenga, kufuatilia, kuchunguza na kukamata wahalifu mbalimbali pamoja na wanaopanga njama za kuiba, kuvunja nyumba, wanaouza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya”amesema SACP Muliro

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI