KAWAIDA - VIJANA KEMEENI MATUMIZI YA MTANDAO WA X
Na Mwandishi wetu, HabariPlus
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida amewataka vijana wa Chama hicho kukemea juu ya matumizi mabaya ya mtandao wa Twitter maarufu kama X nchini Tanzania kutokana na kubadilika kwa maudhui ya mtandao huo.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hivi karibuni wamepokea taarifa ya kushtua kutokana na mtandao huo kubadilisha maudhui yake na kuanza kuruhusu kutumika kwa picha za ngono maarufu kama ponogroph.
Amesema kuwa, picha zinazorushwa kwenye mtandao huo hazina maadili kwa kizazi cha kitanzania hasa ukilinganisha watoto wengi na vijana wamekua wakitumia simu kuingia kwenye mitandao hivyo kuwepo kwa picha hizo mtandao ambapo zinapotosha watoto kufuata na kufanya mambo yasiofaa.
Amesema kuwa, Uvccm wamekua wakua walezi wazuri wa maadili kwa vijana wote hivyo hawapendezwi na mtandao huo kuamza kubadilisha maudhui yake na kuruhusu matumizi ya picha na video za ngono kwani zinaleta athari kwa kizazi cha sasa ni kinachokuja.
"Kwanza hata jina lenyewe tu linalotumika limekua na maudhui yanayoendana na masuala ya kuhamasisha ponograph, watoto wengi wanatumia simu na wanaingia kwenye mitandao, hivyo sio vizuri mtandao huo kutumika nchini kwetu"amesema Kawaida.
Hata hivyo, ameiomba Serikali kuingilia kati jambo hilo na kuufungia mtandao wa twitter maarufu kama X nchini Tanzania usitumike kwani unapotosha maadili na vijana kuanza kuiga mambo ya kigeni yasiofaa ndani ya jamii.
Aidha amesema wao hawana shida na mtandao huo kutumika nchini Tanzania ikiwa wataondoa maudhui yake yasiyofaa basi uendelee kutumika ila kama haiwezekeni basi vyema Serikali ikaufungia kutokana na kuruhusu kurusha maudhui yasiofaa.
Comments
Post a Comment