LHRC YATOA MAPENDEKEZO HAYA KWA SERIKALI


Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC) kimeiomba Serikali kupunguza kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa zote zenye uhitaji mkubwa kwenye matumizi ya nyumbani kama vile bidhaa za Chakula ili kupunguza ukali wa maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo hii Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wakili Fulgence Massawe wakati akitoa maoni ya kituo hicho, kuhusu bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/25 ambapo amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili mfululizo kutokana na sababu mbalimbali za siasa za ulimwemguni gharama za maisha zimepanda.

"Gharama za maisha zimepanda kwa miaka miwili mfululizo ikilinganishwa na kipindi kabla ya miaka miwili, msingi wa mapendekezo haya unaendana na ibara ya 14 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , 1977 inayobainishwa haki ya kuishi"amesema Wakili Massawe.

Amesema kuwa, makadirio ya mapendekezo ya bajeti ya Serikali yamekuwa ya matumizi ya  kawaida zaidi kuliko maendeleo ambapo asilimia 70 ni matumizi ya kawaida na 30 ndio imeelekeza kwenye maendeleo.

"Kutokana na makadirio ya bajeti hii wananchi wasitegemee miradi mipya wala maendeleo makubwa kwani bajeti hiyo ni ya matumizi ya kawaida na kulipana mishahara pamoja na madeni"amesema Wakili Massawe.

Ameongeza kuwa, "Matumizi mengine ya kawaida yamekuwa ni ya anasa ambayo ni pamoja na magari ya kifahari na watendaji wakuu wa nchi kuishi Dar es Salaam muda mwingi kuliko Dodoma hali inayosababisha kuhudumia miji mikuu miwili ambapo ni gharama kubwa".

Amesema kuwa, kwa mujibu wa bajeti hiyo vyanzo vya mapato vimeendelea kuwa vile vile huku wanaochangia bajeti kwa njia ya kodi ni wananchi wachache.

Hata hivyo, amesema vyanzo vya mapato vimekua sio endeleevu kwani watanzania wakiamua kubadilisha mfumo wa maisha na kuacha kunywa na kuvuta ina maana nchi itashindwaa kujiendeleza.

“Kuna haja ya Serikali kubuni vyanzo vipya vya mapato, mfano mchango wa Halmashauri kwenye bajeti yetu ni mdogo sana, Halmashauri nazo zimeshindwa kubuni vyanzo vipya mfano kupima ardhi kwa wingi na kumilikisha wananchi ili kupata kodi ya ardhi" amesema Wakili Massawe.

Akizungumzia kuhusu deni la Serikali amesema bado linaendelea kuongezeka kama ilivyoainishwa katika taarifa ya hali ya uchumi 2024 na mpango wa maendeleo ya Taifa, 2024/25 iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof Kitila Mkumbo.

Amesema kuwa, deni hilo limefikia shill trilion 91.7 mwezi March 2024 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo deni hilo lilikua trillion 69.44 kutoka trillion 60 .72 kwa mwaka 2021.

Katika hatua nyengine amesema kumekua na uhaba mkubwa wa pesa za kigeni nchini ambapo Serikali imeshindwa kutambua chanzo cha uhaba huo kwani Serikali imepiga marufuku matumizi ya pesa ya pesa za kigeni kitu ambacho kitahatarisha matumizi hayo na hali kuwa mbaya zaidi kwani pesa hizo zinauhitaji mkubwa kwenye taifa la Tanzania .

"Serikali lazima iwe na mkakati ya kujenga mazingira rafiki na kuhamasisha wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza nchini kwetu, mazingira yanayokwamisha wawekezaji Tanzania yanajulikana lakini wanashindwa kuyachukulia hatua stahiki "amesema Wakili Massawe.

Aidha, Lhrc inaipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kugharamia bima ya afya kwa wote kwa kutafuta vyanzo vya fedha ya kugharamia bima hiyo, huku ikipendekeza kuongeza uwazi na uwajibikaji juu ya ukusanyaji na utumiaji wa fedha hizo.

Hata hivyo, lhrc imependekeza kupngeza wigo wa nafuu ya kodi kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yameweza kutimiza masharti yote ya kikodi tangu kuanzishwa kwake, lengo ikiwa ni kupungiza gharama za uendeshaji wa mashirika hayo hasa yanayotoa huduma ya kisheria kwa wananchi wasiokuwa na uwezo nchini.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...