MCHAMBUZI WA SIASA AMJIA JUU MBUNGE MPINA KUHUSU SAKATA LA KUMUITA WAZIRI BASHE FISADI


Msomi na Mchambuzi wa maswala ya  Siasa na uchumi Nchini, Kasim kibao amemjia juu mbunge was kisesa  Luhaga Mpina kwa kitendo chake cha kupotosha umma  juu ya shutuma alizozitoa kwa Waziri wa kilimo na Chakula Hussein Bashe ambapo amemshutumu kwa kumuita fisadi kufuatia kutoa vibari vya uagizaji sukari kwa wafanyabiashara.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini dar es salaam, Kibao amesema kitendo alichofanya mh.mpina ni kukosa subra kwani alipaswa kufuata ushahuri wa Mheshimiwa spika bunge la jamhuri ya Muungano WA Tanzania Turia Akson ambaye alimtaka kuleta ushahidi juu ya shutuma hizo na nyingine mbalimbali.

katika hatua nyingine Kibao amemesa kitendo kinachofanywa na mbunge huyo ni kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo amesema ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi.

Hata hivyo,  amesema anachokifanya Mhe. mpina ni kutafuta huruma kwa Wananchi jambo ambalo amesisita kuwa halina afya kwa Taifa

Aidha Kibao amefafanua kuhusu sakata Mheshimiwa Waziri kilimo mh bashe ambaye aliigaziy Wizara ya kilimo kutoa vibari kwa wafanyabiashara wa viwanda ili Kuokoa hali ya sukari Nchini katika kipindi cha mwezi mtukufu WA Ramadhan na kwarezima.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI