RAIS FILIPE NYUSI KUZURU TANZANIA SIKU 4
Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar
Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi anatarijiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku 4 ambapo pamoja na mengine anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba saba) ambayo atayafungua Julai 3, 2024.
Akizungimza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Januari Makamba amesema kuwa Rais Filipe Nyusi anakwenda Tanzania kwa mwaliko wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa, Rais Nyusi anakwenda nchini humo kwa sababu mbili ya kwanza ziara ya kitaifa ambapo atakutana na Rais Samia ikulu jijini Dar es Salaam ambapo watajadili mambo mengi ikiwemo na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili ili kuimarisha mahusiano yao.
"Rais Filipe Nyusi anakuja nchini kwetu kwa ziara ya siku nne kwa sababu ya kufungua maonyesho ya sabasaba na ziara ya kitaifa ambapo atawasili tarehe 1 atapokelewa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere na viongozi mbalimbali wa Serikali lakini tarehe 2 atapokelewa rasmi na mwenyeji wake ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan "amesema Waziri Makamba.
Ameongeza"Marais hawa wawili watakutana faragha kuzungumza wao wawili, badae watakutana na viongozi mbalimbali ambapo pamoja na mambo mengine baada ya kufanya mkutano na viongozi pia watazunguza na waandishi wa habari"amesema
Hata hivyo, amesema pia katika ziara hiyo watasaini mikataba ya ushirikiano katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu pamoja na mashirika ya habari lengo ni kueka mahusiano mazuri hasa katika kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi ya Msumbiji pamoja na kukuza mahusiano ya kibiashara.
Sambamba na hayo amesema kuwa ujazo wa biashara katika nchi hizo bado sio nzuri kwani biashara zinafanyika mpakani na hazirikodiwi ambapo Tanzania ndio imekua ikiuza bishara nyingi zaidi Msumbiji kuliko nchi hiyo kuuza Tanzania.
Hata hivyo, amesema tarehe 3 Rais Nyusi atafungua maonyesho hayo na baadae mchana atakwenda Zanzibar kwa ajiki ya ziara binafsi pia kupitia ziara hiyo Rais Nyusi atawaaga watanzania kwani muda wake wa kukaa madarakani umeisha, hivyo ziara hiyo itakua ndio ya mwisho nchini Tanzania, huku nchi hizo zikiwa na historia ya ukaribu .
"Nchi ya Msumbiji ilikua inakabiliwa na changamoto ya ulinzi na usalama kutokana na ukaribu tulionao tulipeleka jeshi letu kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama nchi mwao, hivyo ziara hii itaimarisha mahusiano mazuri yaliopo baina yetu"amesema Waziri Makamba.
Comments
Post a Comment