SGR KUANZA SAFARI RASMI KESHO

 

Na Mwandishi wetu,HabariPlus

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limezindua rasmi kampeni ya kuanza safari kwa treni ya kisasa ya SGR yenye kiwango cha kimataifa   June 14, 2024 kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa bei ya sh 13000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Massanja Kadogosa amesema kuwa uzinduzi rasmi utafanyika Juni 25 mwaka huu ambapo utazinduliwa na Rais Dkt Samia Suluh Hassan.

Amesema kuwa, uwepo wa treni hiyo utarahisisha usafiri kwa wananchi kwa gharama nafuu zaidi na usalama wa hali juu ambapo abiria watakapokuwa kwenye treni hiyo watafurahia huduma bora zitakazotolewa na wahumu .

Aidha, amesema ujio wa reli ya kisasa SGR haijaja kuchukua nafasi ya basi, reli ndege wala treni ya zamani bali ni mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ya taifa.

Hata hivyo, amesema wameshirikiana na Tanzania Commercial Benk (TCB) katika suala zima la ukatishaji wa tiketi ambapo wateja watatumia benki hiyo kufanya malipo ya tiketi, na wengine watafika kwenye madirisha ya ofisi hizo kukata titeki.

Aidha, amewataka wananchi kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo, huku akiahidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watu wote watakao haribu miundombinu hiyo.

"Hizi ni kodi za wananchi hivyo wanatakiwa waitunze, wasiharibu moundombinu tutafunga kamera za usalamana tutaweza walinzi kila sehemu ili kuangalia na tutakua na chumba maalum cha kuangalia taarifa zote inapokua njiani"amesema Kadogosa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanzania Commercial Benki TCB, Adam Mihayo amesema kuwa uzinduzi huo ni mabadiliko makubwa katika mapinduzi ya kiuchumi nchini Tanzania .

Aidha amesema kuwa wanafuraha kubwa kuwa sehemu ya ushirikiano huo ambao unaakisi matarajio makubwa ya wananchi katika kutekeleza reli ya kiwango cha kimataifa .

"Tumeingia makubaliano ya kutoa huduma ya malipo kwa wateja katika ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao ambapo malipo hayo yatakwenda kusaidia katika mashirikiano yao "amesema Mihayo.

Naye, Afisa Biashara kutoka TRC amesema kuwa abiria watakaosafiri katika reli hiyo hawatoruhusiwa kubeba vyakula wala mizigo mikubwa ambapo kwa daraja la kawaida watabeba mzigo wa kilo 20 bure.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI