HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na Wakulima, Wafugaji, Mamlaka za wanyamapori , Mamlaka za maji na Afya waendelee kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalamu katika sekta husika ili kujiepusha na athari za mvua zinaponyesha. Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 31,2024 Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili 2025. Amesema kuwa, mvua za msimu ni mahususi katika maeneo ya Magharibi mwa nchi Kanda ya kati, Nyanda za juu kusini Magharibi kusini, ukanda wa Pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambapo maeneo hayo yanapata msimu mmoja kwa mwaka. Aidha, kutokana na mifumo ya hali ya hewa, mvua za wastani hadi chini wastani zin...
Comments
Post a Comment