VIONGOZI WA DINI WAIOMBA SERIKALI KUUFUNGIA MTANDAO WA X
Viongozi wa Dini nchini Tanzania wamezitaka mamlaka za Serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa Twitter maarufu kama X kwa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga)
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Alhaj Dkt Abdul Suleiman amesema mtandao huo umekua ukihamasisha vitendo vya ushoga, jambo ambalo limepigwa vita vimepigwa vita hata katika maandiko ya dini.
Dkt Sule amesema kuwa, kufuatia mtandao wa X (Twitter) kuruhusu kuchapisha maudhui yanayohamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji mamlaka zinazohusiana na mawasiliano zinatakiwa kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuufungia kabisa mtandao huo.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Kanisa la Methodox Tanzania Askofu Allen Siso amesema katika vitabu vya dini zote havikubaliani na ndoa za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili na wanaume nao vivyo hivyo'.
Naye, Sheikh Hilal Kipozeo amesema mtandao wa X unabidi kufungiwa haraka iwezekanavyo na ni vyema kutengenezwa sheria kali ya kudhibiti mapenzi ya jinsia moja na usagaji ili kusaidia kizazi kijacho kisiharibike.
"Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka hivyo Mara moja mtandao wa X ufungiwe"amesema
Munira Njau ni mwalimu wa shule ya Msingi Gongolamboto Manipsaa ya Ilala amesema kuwa imekua ni kero kubwa sana mashuleni kwa watoto kuweza kufanya mambo yasiofaa, hivyo kuwepo kwa mtandao huo kutasababisha athari kubwa kwa jamiii.
Amesema kuwa wazazi wamekuwa na tabia za kuwaachia watoto wao wachezee simu zao hali iliyopelekea watoto kuingia kwenye mitandao hiyo na kujifunza tabia mbaya siku hadi siku na hatimaye kuzipeleka mashuleni.
"Sisi walimu tunashinda na watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni,na tunakutana na wanafunzi ambao tayari wana viashiria vya tatizo hilo na tunapowahoji wanasema wamekuwa wakisema vimeanzia majumbani na wengine kupitia simu za wazazi wao, hivyo suala hili tuungane wote kusaidia watoto.
Comments
Post a Comment