SERIKALI KUWALIPA WANAOPISHA MIRADI YA MAENDELEO
Na Mwandishi wetu
Serikali imesema imekua ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha wananchi wanaopitiwa na miradi mbalimbali ya kimaendeleo wanalipwa stahiki zao katika maeneo yaliopitiwa na miradi ili kuhakikisha hakuna malalamiko kutoka kwa wananchi.
Akizungumza na wadau mbalimbali, Kamishana wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nyanda Shuli, katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya HakiRasilimali ambapo amesema Tume hiyo imekua ikifanya kazi na wadau mbalimbali.
"Tume ya haki na utawala bora imekuwa ikifanya kazi na wadau mbalimbali ikiwemo kituo cha Sheria na haki za Binadamu(LHRC) na imekuwa ikipokea malalamiko ya aina tofauti tofauti kutoka kwa wananchi nakuyaripoti Mahakamani kupatiwa utatuzi"amesema Nyanda.
Aidha, katika mdahalo huo walijadili kwa kina namna sheria zinavyoweza kumsadia mwananchi kupata haki zake pale mradi unapopita katika eneo lake ili aweze kulipwa fidia kulingana na hali halisi ya mali zilizopo
"Kuna baadhi ya mikanganyiko inayotokea wengine kutoridhika na fidia wanazolipwa hivyo kuamua kupeleka malalamiko mahakamani,hivyo inatakiwa elimu iendelee kutolewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali"amesema Shuli
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Mradi wa Bomba la Mafuta Gafi kutoka Unganda hadi Tanzania(ECOP) Fatma Msumi amebainisha kuwa baadhi ya maeneo ambayo bomba hilo limepita Wananchi wamepatiwa stahiki zao kwa mujibu wa sheria za haki za Binadamu.
"Vingine ilitulazimu kukutana na wazee wa kimila kwanza kuzungumza nao kutokana na baadhi yao imanani zao na matambiko yao hufanyika kwenye makaburi au miti hivyo wengine kukataa kabisa kuhamisha makaburi yao na kuwalazimu wao kuangalia namna ya kukwepa maeneo hayo ili kusitokee mkanganyiko' amesema
Nakuongeza kuwa "Kiukweli Mradi huu wa bomba la mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kila maeneo ramani yake imeonyesha litapita kuna ofisi ambayo watumishi wake wamekuwa wakizungumza na viongozi wa kijiji, kitongoji ,kimila kuweka mazungumzo ya pamoja kuhusu raslimali zao kama kuna uwezekano wa kulipwa fidia wapishe maradi "
Kwa upande wake,Mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu kutoka kituo cha Sheria na haki za binadamu LHRC, Joyse Komanya amesema kituo hiko kimekuwa kikipokea malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu haki raslimali kwa wanaopisha miradi kwani wengine hulipwa fidia ndogo ikilinganishwa na mali walizonazo hivyo nao wamekuwa wakiwasaidia kwa kuwapatia Elimu namna ya kupata haki zao
Comments
Post a Comment