TAMISEMI KESHO KIKAANGONI, WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA MAHAKAMA KUU DAR

 



Na Mwandishi wetu 

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kesho saa 8 mchana katika mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam kuskiliza hoja za mwanasheria mkuu wa Serikali kuhusu kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa vitongoji vijiji na Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika mweiz Novemba mwaka 2024.

Shauri hilo limefunguliwa na wananchi watatu ambao ni raia wa kitanzania dhidi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimamia uchaguzi wa mwaka huu (2024) wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii Dkt Ananilea Nkya ambaye ni miongoni wa wnanchi hao amesema kuwa maombi hayo  yatasikilizwa Jumatano wiki hii Agost, 28 Agosti 2024 katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo yatarushwa moja kwa moja  (mubashara) kupitia vyombo mbali mbali vya habari.

Dkt Nkya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) amesema kuwa maombi hayo yalitajwa kwa mara ya kwanza Agost 22,2024, 
 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa akili ya kusikiliza kesi hiyo na kuwa sehemu kwani wanachokifanya wao ni kutetea haki ya watanzania.

"Shauri hili namba 19721 ya 2024 mbele ya Jaji Dyansobera yalipotajwa Mahakamani kwa mara ya kwanza, Jaji Dyansobera aliwapa wanasheria wa Serikali siku saba, kati ya Agosti 22 na 28 2024, kuleta hoja za Serikali mahakamani ili mahakama izisikilize, kupima na  kutoa maamuzi kuhusu maombi ya raia kuzuia TAMISEMI kujihusisha na uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji." amesema Dkt Nkya

Ameongeza"Sisi raia tuliopeleka maombi ya kufungua shauri la Kikatiba Mahakama Kuu tunaamini kuna umuhimu mkubwa  kwa wananchi kufika kwa wingi Salaam siku ya Jumatano, Agosti 28, 2024 kuskiliza, raia watapata fursa  ya kusikiliza hoja za Serikali moja kwa moja kutoka kwa wanasheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hoja za raia kupitia kwa Mawakili wetu kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi"

Kwa upande wake, Bob Wangwe ambae ni miongoni mwa raia hao waliofungua kesi ya kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa amesema kuwa wamefungua shauri hilo kwa kuwa wanatambua raia ndio  mamlaka ya nchi kama inavyothibitishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ibara ya 8(1)(a).

Ibara hii 8(1)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii.

 "Sisi raia  kwa mamlaka tuliyonayo kwa mujibu na Katiba tunapinga Tamisemi kusimamia uchaguzi kwani tunaona ni kinyume cha katiba na sheria za nchi iwapo TAMISEMI itasimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kwani itakua inahodhi mamlaka ya Tume huru ya uchaguzi".

 Aidha ameongeza kuwa, kifungu cha 10(1)(c) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Namba 2 ya 2014 kinatoa wajibu na mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kwa Tume, siyo TAMISEMI. 

Bob Wangwe ambae pia ni Mkurugenzi wa JUKATA amesema uchaguzi ukisimamiwa na mamlaka isiyohusika kuna hatari ya uchaguzi huo kutokuwa na unyoofu, huru na haki  na athari zake ni pamoja na kusababisha vijiji, mitaa na vitongoji kuongozwa na watu wasiowaadilifu na wasiowajibika kwa raia, hata kufuja michango na kodi za wananchi.

"Msingi wa kisheria wa kesi hii
maombi ya kesi yanahoji kwamba Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kusimamia uchaguzi kunaleta hatari kubwa kwa haki na uwazi wa mchakato wa uchaguzi, matukio ya awali ya dosari na upendeleo unaoonekana ndani ya Wizara yamezua maswali juu ya uwezo wake wa kusimamia uchaguzi huu bila upendeleo"amesema Bob Wangwe

Nae Bubelwa Kaiza ambaye ni moja wa wananchi hao amesema kuwa hatua hiyo ya kisheria inalenga kulinda haki ya kikatiba ya raia wa Tanzania kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia ambao ni nyoofu, huru na wa haki.

Amesema, baada ya kutungwa kwa sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ibara ya 74(6)(e) majukumu ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, kamati za mitaa na wenyeviti wa Vitongoji yako chini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

"TAMISEMI kutaka kusimia uchaguzi huu ni batili na kinyume cha sheria, kwa mujibu wa kifungu cha 1 0(1)(c) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi pekee yenye jukumu la kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, kamati za mitaa na wenyeviti wa Vitongoji.

Ameongeza kuwa, madhara ya kukosekana viongozi halali kwenye mitaa, vijiji, na vitongoji tunahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kufuatilia na kusikiliza maombi ya kesi hii mahakamani kwa sababu uchaguzi usipoendeshwa kwa mujibu wa Katiba, sheria na uadilifu raia wataendelea kukabiliwa na changamoto za maendeleo pasipo msukumo wa uongozi kuwajibika kuzishughulikia.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI